
UFUNUO CHANNEL
February 9, 2025 at 07:37 PM
_Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu. - Ufunuo 7:4_
Tangazo la idadi ya wale waliotiwa muhuri linaashiria ukamilishwaji wa hatua hiyo. Yohana anasikia kwamba idadi yao ni 144,000 kutoka katika makabila 12 ya Israeli. Rejea hii haihusu tarakimu halisi bali kile inachoashiria. Tarakimu hii (144,000) inaundwa 12 mara 12 mara 1,000. Kumi na mbili ni ishara ya watu wa Mungu: makabila ya Israeli na alama ya kanisa likiwa limejengwa juu ya msingi wa mitume 12 (Efe. 2:20). Hivyo, tarakimu 144,000 huwakilisha utimilifu wa watu wa Mungu wa siku za mwisho, udhihirisho wa kisasa wa Israeli ya zamani.
Makabila 12 yaliyoorodheshwa katika Ufunuo 7 si ya kihistoria, kwa sababu makabila 12 ya Israeli hayapo leo. Makabila 10 yalichukuliwa utumwani wakati wa shambulio la Waashuri (2 Wafalme 17:6–23), ambapo walichangamana na mataifa mengine. Makabila 12 hayaundi dini ya Kiyahudi leo.
Orodha ya makabila 12 ya Ufunuo 7 si orodha yenye mpangilio wa kawaida. Yuda anaorodheshwa kama kabila la kwanza badala ya Reubeni. Pia, makabila ya Dani na Efraimu yameondolewa, na Yusufu na Lawi yamejumuishwa badala yao. Sababu bayana ya kuondolewa kwa Dani na Efraimu ni kwa vile katika Agano la Kale makabila mawili haya ni waasi na waabudu-sanamu (Amu. 18:27–32, Hos. 4:17).
Orodha ya makabila katika Ufunuo 7 si ya kihistoria bali kiroho. Hutuambia kwamba ukosefu wa uaminifu kwa makabila ya Dani na Efraimu hauna nafasi miongoni mwa watu wa Mungu waliotiwa muhuri. Pia, kanisa katika Agano Jipya hutajwa kama makabila 12 ya Israeli (Yakobo 1:1). Makabila 12 katika Ufunuo 7 huwakilisha watu wa Mungu wote, Wayahudi na Wamataifa.
Hawa 144,000 wanaoneshwa kama jeshi lililoundwa kwa mfumo wa Israeli ya zamani wakienda vitani. Katika Israeli ya zamani, palikuwa na askari 1,000 katika kombania moja ya jeshi (Hes. 31:3–6). Namba 144,000 ya ishara huonesha kanisa lililoko vitani kwa namna ya kombania 144 za kijeshi zenye askari 1,000 waliotayari kwa ajili ya vita vya mwisho (Ufu. 17:14), tofauti na jeshi la adui lenye idadi ya milioni 200 (Ufu. 9:16).
🙏
2