UFUNUO CHANNEL
UFUNUO CHANNEL
February 16, 2025 at 07:31 PM
_Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba. Ufunuo 8:2_ Katika kuonesha hatua za Mungu za kuingilia kati kwa niaba ya watu Wake, Ufunuo hutumia vielelezo vya tarumbeta katika Agano la Kale. Tarumbeta vilikuwa vyombo muhimu vya maisha ya kila siku ya Israeli ya zamani (angalia Hes. 10:8–10 , 2 Nyak. 13:14, 15). Sauti zake ziliwakumbusha watu juu ya ibada hekaluni; tarumbeta zilipulizwa pia katika vita, wakati wa mavuno, na wakati wa sikukuu. Upulizaji wa tarumbeta uliambatana na maombi. Wakati wa ibada hekaluni au wakati wa sikukuu, tarumbeta “zilimkumbusha” Mungu juu ya agano Lake na watu Wake. Pia ziliwakumbusha watu wawe tayari kwa ajili ya “siku ya Bwana” (Yoeli 2:1). Wakati wa vita, sauti ya tarumbeta, iliyoambatana na maombi, ilimwita Mungu awaokoe watu Wake. Dhana hii ni msingi wa tarumbeta katika Ufunuo. Tukio lililoashiriwa kwa tarumbeta katika Ufunuo hudokeza juu ya hatua ya Mungu ya kuingilia kati katika historia kama jibu la maombi ya watu Wake. Wakati ambapo kimsingi muhuri unawahusu wale wanaodai kuwa watu wa Mungu, tarumbeta hutangaza hukumu dhidi ya wakazi wa dunia (Ufu. 8:13). Wakati huohuo, haya ni maonyo kwa watu ili kuwaleta katika toba kabla hawajachelewa kabisa. Tarumbeta saba hukamilisha historia nzima tangu wakati wa Yohana hadi hitimisho la historia ya dunia hii (Ufu. 11:15–18). Zinapulizwa ilhali maombezi yakiendelea mbinguni (Ufu. 8:3–6), na injili ikihubiriwa duniani (Ufu. 10:8–11:14). Hukumu za tarumbeta hizi ni kwa sehemu tu; huathiri theluthi tu ya uumbaji. Tarumbeta ya saba hutangaza kwamba muda umewadia kwa ajili ya Mungu kutwaa utawala Wake stahiki. Tarumbeta saba zinahusika takriban katika vipindi husika vinavyohusika na makanisa saba: Tarumbeta mbili za kwanza hutangaza hukumu juu ya mataifa yaliyomsulubisha Kristo na kulitesa kanisa la awali, Yerusalemu mwasi, na Himaya ya Rumi. Tarumbeta ya tatu na ya nne huonesha mwitikio wa mbingu kwa uasi wa kipindi cha zama za kati na baada ya Matengenezo. Tarumbeta ya tano na ya sita huelezea hali katika ulimwengu wa kipagani baada ya Zama za Maarifa, zinazobainishwa kwa utendaji mkubwa wa nguvu za kishetani zinazoukusanya ulimwengu kwenye vita vya Har-Magedoni.

Comments