
UFUNUO CHANNEL
February 23, 2025 at 08:10 PM
_Mikononi mwake alishika kitabu kidogo kimefunguliwa. Aliweka mguu wake wa kulia juu ya bahari na wa kushoto juu ya nchi kavu, Ufunuo 10:2_
Tarumbeta ya sita hutufikisha katika wakati wa mwisho. Watu wa Mungu wanatakiwa kufanya nini katika wakati huu? Kabla tarumbeta ya saba haijapulizwa, tukio fulani linaingizwa, likielezea jukumu na uzoefu wa watu wa Mungu katika wakati wa mwisho.
Malaika huyu mwenye umbo la Kristo, ameshikilia kitabu wazi. Anaweka miguu Yake baharini na nchi kavu, ikiashiria utawala Wake wa ulimwengu mzima, na kwamba kile anachokaribia kutangaza kina umuhimu wa ulimwengu wote. Anapaza sauti kwa ngurumo ya simba. Ngurumo ya simba huwakilisha sauti ya Mungu (angalia Hos. 11:10).
Yohana haruhusiwi kuandika yale yaliyotamkwa kwenye ngurumo hizo. Yapo mambo yanayohusiana na wakati ujao ambayo Mungu hajayafunua kupitia Yohana.
Malaika anapotamka kwamba “hapatakuwa na wakati baada ya haya” (Ufu. 10:6), neno la Kiyunani chronos huonesha kwamba anazungumzia kipindi cha wakati. Hili huelekeza huko awali katika Danieli 12:6, 7, ambapo malaika anasema mateso ya watakatifu yatadumu kwa wakati, nyakati, na nusu wake, au miaka 1,260 (538–1798 B.K.). Wakati fulani baada ya kipindi hiki cha kinabii, mwisho ungewadia.
Kauli kwamba hapatakuwa na wakati tena huzungumzia unabii wa wakati katika Danieli, hasa siku 2,300 za kinabii za Danieli 8:14 (457 K.K.–1844 B.K.). Baada ya kipindi hiki, hakutakuwepo tena vipindi vya kinabii.
❤️
1