
Francis | Abracadabra
February 22, 2025 at 02:37 PM
Huu Sio Uchawi,
Chochote Utakacho Nuia,
Kwa Kumaanisha Na Ukafanya,
Hivi Kwa Siku Kadhaa…
( Spell ) Kinatokea.
How?...
Case Study:
1• Waganga wa Kienyenyi:
Kafara Haiwezi Kuwa Kafara Iliyokamilika,
Bila Kuitamkia Maneno.
....Wanaita ( Kinuiza ).
Maneno Yana Nguvu Ya Kuumba,
Kitu Katika Ulimwengu ( Universe ).
Na Hii Nguvu Amepewa,
Mwanadamu Yeyote Yule.
...
2• Watumishi wa Mungu:
Hawa Wengi Wanaijua Siri hii,
Iliyopo Kwenye Maneno…
Huitumia Sana Ku-spell
“Kunuiza”
Hii Ni Mifano Miwili Iliyoo Hai!
...
Ok,
Labda Nitumie Njia Hii Utanielewa!
Neno Lolote Utakalo Tamka,
Linaashiria (Mawasiliano)
Mfano 1 : Ukimwambia Mtoto Mdogo.
"Nenda Kaniletee Mwiko Upo Pale Jikoni"
Hapa Tayar Umeumba Kitendo,
Na Kinaenda Kufanyika Kama Ulivyo Tamka.
...
Nirudi, Kwenye Kusudi La Andiko Hili.
Unaweza Una "Nuia" Chochote Kile,
Na Kikafanyia Kwa Njia Usizotarajia.
Maneno Yako Ndio Silaha Tosha,
Ya Kukupa Chochote Unachotaka!
Sasa Inategemea Wewe,
Unayatumiaje Ulimi Wako...
Jitahidi Kila Neno Unalo - Tamka,
Liwe Na Maana Kwako Mwenyewe Kwanza.
...
Zungumza Inapobidi,
Uwezo Wa Ku-Control Kila Kitokacho,
Mdomoni Kwako Upo Kwako Mwenyewe.
Namalizia Kwa Kusema!
Mithali 18: 21
↳ "Mauti Na Uzima Huwa Katika Uwezo Wa Ulimi"
Jitamkie Mambo Mazuri na Uzima!
...
^Abracadabra^
❤️
👍
🙏
🫡
💪
29