MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 4, 2025 at 02:12 PM
*MUKHTASAR WA FUNGA* ____________________ No. 0️⃣4️⃣ *NAFASI YA FUNGA* Funga ya Ramadhan ni nguzo ya nne miongoni mwa nguzo za uislamu. Allaah ameifaradhisha katika mwezi wa pili wa hijra, na kwa utukufu wa nafasi ya funga Allaah ameifaradhisha juu ya umma huu na umma zengine kabla yake, na kwa hakika amefunga Mtume swala na salamu ziwe juu yake Ramadhan tisa. *FADHLA ZA FUNGA YA RAMADHAN* 1.Mwezi wa Ramadhan ndio mwezi ambao imeteremshwa Qur-an ndani ya usiku mtukufu [Laylatul Qadr], kupitia Malaika mtukufu [Jibri], kwenda kwa Mtume Mtukufu [Muhammad - Swalla llaahi 'alayhi wasallama] katika mji mtukufu [Makka] kwa umma mtukufu na kwa lugha tukufu [Kiarabu]. Qur-an ambayo ndiyo muongozo na kibainifu kwa watu, ni ibada kuisoma kwake bali mtu hulipwa fadhla nyingi tu - kwa kila herufi moja anayoisoma. 2.Unapofika mwezi wa Ramadhan hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto pamoja na kufungwa mashetani. 3.Malipo makubwa ya funga na ni sababu ya mtu kusamehewa makosa yake - kwani yeyote atakayeifunga Ramadhan kwa imani na kutarajia malipo mbele ya Allaah basi husamehewa makosa yake yaliyotangulia. 4.Mfungaji huwa na furaha mbili - moja ni pale anapofuturu na nyengine ni pale atakapokutana na Mola wake mlezi. 5.Allaah amejiegemezea funga na yeye ndiye atakayeilipa, pamoja matendo yote anayelipa ni Allaah. 6.Miongoni mwa milango nane ya peponi kuna mlango unaitwa Rayyan mlango huo hatoingia yeyote isipokuwa wale waliofunga. Baaraka llaahu fiikum ______________ ✍️Abuu Muyassam Alkujaaniy

Comments