
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 5, 2025 at 11:19 AM
Amesema Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama:
*"FUNGENI MILANGO, NA TAJENI JINA LA ALLAAH; KWANI HAKIKA YA SHETANI HAFUNGUI MLANGO ULIOFUNGWA"*
____________________
*📚 Swahihul Bukhary [3304]*
*********
Haya ni katika mafunzo tuliyofunzwa na Mtume wetu katika namna ya kujikinga na shetani, ametuelekeza Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama kuwa inapofika jioni muda wa jua kuzama : Tuwafungie watoto wetu ndani na tufunge milango na kufunikiza vyombo na kuvifunga vyengine.
Muhimu sana kwa muislamu kupa umuhimu sana haya maelekezo na mafunzo ya Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama tusiwaachie hovyo watoto wetu muda huo na tusibakishe milango na vyombo wazi.
Baaraka llaahu fiikum
____________
✍️ Abuu Muyassam Alkujaaniy