MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 6, 2025 at 03:54 AM
🤏 *SWALA !!! SWALA !!! SWALA!!*👌 _____________ "Nawausia ndugu zangu sambamba na kuiusia nafsi yangu tumche Allaah - kwa kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake. Suala la *swala* ndugu zangu linapuuziwa sana hasa kwenye mazingira manne: *1. KAZINI:* watu wengi wakiwa makazini kwao hupotezea suala la swala, ima huswali nje ya wakati au huacha tu kuswali. Huu sio udhuru. *2.MSIBANI:* pamoja na huzuni zinazotanda kwenye misiba kwa kuondokewa na mmoja wa vipenzi vyetu lakini lisizuie jambo hili kutekeleza haki ya Allaah. Hapa utakuta kuanzia aliyefiwa na wengine waliokuja pale swala hupuuzwa na hakuna wa kumkumbusha mwenziwe. *3. HARUSINI* Sasa hivu maharusini kumekuwa viwanja vya fujo na maasi - achilia mbali mziki, kucheza na kuvaa hovyo - bali swala husahaulika kabisa kuanzia kwa bibi harusi na bwana harusi na wengine wote hasa hasa wanawake, mtihani mtupu. *4. SAFARINI:* Wengi wetu tukiwa tunasafiri pamoja na kupewa ruhusa ya kupunguza swala au kukusanya lakini mtu huianza safari yake hata ikiwa ya mchana kutwa au usiku kucha akapitwa na swala zote wala hajali. Tujitahidini ndugu zangu kwa kila mmoja na nafasi yake kwani sote ni wachunga na tutaulizwa sote, tuelimishane tukumbushane - mtu aulizie hasa nyumbani mmeswali au aamrishe watu kwenda kuswali sio kuwaacha tu - wakike kwa wakiume wadogo kwa wakubwa. Baaraka llaahu fiikum __________________ ✍️ Abuu Muyassam Alkujaaniy
👍 1

Comments