MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 7, 2025 at 04:33 AM
*MUKHTASAR WA FUNGA* _____________________ No. 0️⃣6️⃣ *●KUTHIBITI KUINGIA MWEZI WA RAMADHANI* Huthibiti kuingia mwezi wa Ramadhan kwa moja kati ya mambo mawili: 1.Kuonekana mwezi mwendamo wa Ramadhan kutoka kwa muislam, muadilifu, mwenye uwezo wa kuona wakiume au wakike. 2.Kukamilisha mwezi wa Shaaban siku thelathini muda ambao haukuonekana mwezi wa Ramadhan. Dalili; Amesema Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama: "Fungeni kwa kuonekana kwake [mwezi mwendamo wa Ramadhan] na fungueni [mfuturu] kwa kuonekana kwake [mwezi mwendamo wa shawwal] ikiwa mtazuiliwa juu yenu [kuuona] basi kamilisheni hisabu ya idadi ya mwezi wa Shaaban thelathin" Muttafaqun 'Alayhi *●HUKMU ZA KUONEKANA MWEZI WA RAMADHAN:* 🔸️ Pindi itakapothibitika kuingia mwezibwa Ramadhan itawajibika kuanza kufunga. 🔸️Na ikitokea haukuonekana wa Ramadhan pamoja na anga kuwa angavu usiku wa mwezi Thelathini wa Shaaban watakuwa ni wenye kufuturu, na ni hivyo hivyo pale itakapokuwa limezuia wingu au vumbi. 🔸️Na ikiwa watu watafunga siku ishirini na nane kisha wakauona mwezi mwendamo wa Shawwal watafuturu siku inayofuata [yaani itakuwa sikukuu] na itakuwa haramu kufunga. Na itawalazimu kufunga [kulipa] siku moja baada ya Eid . 🔸️Na ikiwa walifunga siku thelathini kwa ushahidi wa mtu mmoja na ukakosa kuuonekana mwezi hawatofuturu mpaka wauone mwezi wa mwendamo wa Shawwal. 🤏 Wanachuoni wamekhitilafiana juu kufunga kila mji na mwezi wake au wafunge kwa mwezi mmoja au kwa nchi zinazoafikiana majira na mawiyo na machweyo 🔸️Atakayeuona mwezi wa Ramadhan peke yake na asikubaliwe kauli yake atafunga kwa siri, na atakayeuona mwezi wa shawwal peke yake na isikubaliwe kauli yake atafuturu siri. ●Yamuwajibikia kiongozi wa waislamu kutangaza kwa njia za kisheria na zinazoruhusiwa kisheria kuingia Ramadhan pale itakapothibiti kuonekana kwa mwezi wake kisheria na pia kutoka kwake. Baaraka llaahu fiikum ___________________ ✍️Abuu Muyassam Alkujaaniy

Comments