MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 9, 2025 at 08:38 AM
*MUKHTASAR WA FUNGA* ____________________ No. 0️⃣7️⃣ *HUKMU YA FUNGA YA ASIYEJUA WAKATI* Ambaye hakujua wakati wa kufunga kama vile kipofu [asiyeona], mfungwa na wengine mfano wao wakakosa kujua wakati wa kufunga watakuwa na hali tatu: 1.Funga yake ikiafikiana na mwezi wa Ramadhan au baada yake funga yake ni sahihi isipokuwa siku ambazo haisihi kufunga. 2.Ikiwa atafunga kabla ya mwezi wa Ramadhan haitosihi funga yake; kwa sababu atakuwa ameleta ibada kabla ya wakati wake. 3.Ikiafikiana funga yake usiku bila kuafiki mchana haitosihi; kwa sababu usiku si wakati wa kufunga. *HUKMU YA MWENYE KUFUNGA KATIKA MJI FULANI KISHA AKASAFIRI:* Ikiwa atafunga muislamu katika mji fulani kisha akasafiri kwenda kwenye mji mwengine, hukmu ya kufunga kwake na kufuturu kwake ni hukmu ya mji ambao amefikia [amekwenda] atafuturu nao pale watakapofuturu. Lakini akiwa huyu msafiri amefuturu chini ya siku ishirini na tisa atalipa siku moja baada ya Eid, na akifunga siku zaidi ya thelathini hatofuturu isipokuwa pamoja nao, na akiwa ni mwenye kurejea nyumbani [kwenye mji wake] atafuturu nao. Na hii imeendana na khilafu iliyopo ya kila mji na mwezi wao au kufunga na kufuturu kwa mwezi mmoja. *HUMKU YA NIA YA FUNGA:* 1.Inamuwajibikiwa kila muislamu ili apate unira basi aifunge Ramadhan kwa iimani na kutarajia malipo mbele ya Allaah, si kwa kufanya riyaa au sum-'aa [kutaka uonekane au usikike] wala isiwe kwa njia ya kufuata mkumbo bali afunge kwa ajili Allaah ameamrisha na kwa ajili ya kutafuta ujira mbele ya Allaah na ni hivyo hivyo ibada zote. 2.Yawajibika kuileta nia ya funga ya wajibu muda wa usiku na kabla ya kuchomoza Alfajir kama vile funga ya Ramadhan na nyenginezo. Na inatosheleza nia moja ni hivyo hivyo kwa mwenye kufunga funga ya kafara ya miezi miwili mfululizo - isipokuwa akiikata funga yake kwa safari. Na jambo hili lina khilafu baina ya wanachuoni wapo wanaoonelea kuwajibika nia katika kila usiku. Tanbiih: Nia ya ibada si sunna kuitamka, kwani hajafanya hivyo Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama wala hajaamrisha si yeye wala maswahaba na wengineo waliofuatia. Nia ipo ndani ya moyo na wala usiitesa nafsi yako kuwa mpaka uniuzwe usiku. Ama funga ya sunna itafaa kuweka nia mchana, pale itakapokuwa hajafanya lolote katika yale yanayoharibu funga kuanzia kuchomoza kwa alfajri ya pili. Tanbiih: Itasihi nia ya funga ya faradh muda wa mchana pale itakapokuwa hakujua uwajibu wake muda wa usiku kama vile lau ilibainishwa bayana kuonekana mwezi wakati wa mchana basi hapo atajizuia muda uliobakia wa siku yake, wala haimlazimu kulipa na hata ikiwa amekula au amekunuwa; ataanza pale alipojua. 3.Inayemuwajibikia funga mchana kama vilr mwendawazimu akapoa, na mtoto mdogo akabaleghe, na kafiri akasilimu na mfano wake, hawa itawatosheleza nia zao wakati wa mchana wakati ilipowajibikia hata ikiwa ni baada ya kula na kunywa wala hawatolipa. 4.Aliyenuia kufunga na akala daku, ukamchukua usingizi na akawa si mwenye kuamka mpaka likazama jua [yaani akalala mchana wote] funga yake ni sahihi wala hatolipa, lakini atakuwa ni mwenye kupata dhambi ikiwa amefanya hivyo kwa kuzembea ni juu yake kuleta istighfaad na kutubia. 5.Atakayeweka nia ya kufuturu ilihali ni mwenye kufunga basi atakuwa ni mwenye kuiharibu funga yake kwa sababu funga imejengwa kwa nguzo mbili : Nia pamoja na kujizuia na vyote vyenye kuharibu funga. Hivyo akinuilia kufuturu atakuwa ameidondosha nguzo ya kwanza ambayo ndiyo msingi wa matendo. 6.Atakayelala usiku wa mwezi thelathini katika mwezi wa Shaaban akajisemea: Ikiwa kesho itakuwa Ramadhan basi mimi nitakuwa mwenye kufunga, kisha ikabainika kuwa ni Ramadhan basi funga yake ni sahihi. Wallaahu a’alaa wa a’alam Baaraka llaahu fiikum Wajazaakumu llaahu khayran ________________________ ✍️ Abuu Muyassam Alkujaaniy

Comments