
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 10, 2025 at 09:41 AM
*MUKHTASAR WA FUNGA*
____________________
No. 0️⃣8️⃣
*HUKMU YA FUNGA KWA MTU MZIMA [WA UMRI] NA MGONJWA:*
1.Yeyote atakayefuturu kwa sababu ya uzee au ugonjwa ambao hautarajiwi kupona - hali akiwa ni mkazi au msafiri - atalisha kila siku masikini mmoja - kwa kiasi cha nusu pishi. Na hilo humtosheleza kutokana na funga yake - yaani hatolipa funga.
▫️ Ima atatengeneza chakula kwa idadi ya siku anazodaiwa na atawaita masikini waje wale , au atawapelekea, naye atakhiyari mwenyewe kulisha kila siku kwa siku yake ama kuchelewesha mpaka siku ya mwisho akalipa zote.
2.Ama atakayepata tatizo la akili - yaani ikamuondoka akili kwa sababu ya uzee - basi huyu hawajibikiwi na funga wala kafara - yaani hatotakiwa kufunga wala kulipiwa funga wala kulisha, kwani anaingia katika hukmu ya wale ambao imenyanyuliwa kalamu - si katika wale wenye kulazimikiwa na sheria [Mukallafiina].
*Tanbiih:* Mwenye ugonjwa ambao hautarijiwi kupona - kwa sababu ya virusi vyake tu na sio kwa athari ya maradhi yenyewe mwilini - yaani ameathirika na virusi vya ugonjwa fulani lakini kufunga anaweza - huyu ima atafunga au kama hawezi kufunga atalipa baadae au kulisha, kama ilivyo kwa mgonjwa wa kawaida.
*Tahadhari:* Tusimdanganye Allaah na waumini kwa kujitia magonjwa ya uongo pale tu inapofika Ramadhani - mara vidonda vya tumbo na kadhalika.
Ibada hii yeye Allaah amesema ni yake na yeye ndiye atailipa. Hivyo yeye ndiye humjua nani mkweli na nani muongo, bali ukijitia kudanganya na kucheza shere basi hakuna unayemdanganya isipokuwa nafsi yako.
*HUMKU YA FUNGA KWA MWENYE HEDHI NA MWENYE NIFASI:*
● Ni haramu juu ya mwenye hedhi na mwenye nifasi kufunga , bali watafuturu na watakujakulipa hapo baada ya Ramadhan.
● Ikiwa watatoharika muda wa mchana, au kwa msafiri ambaye amefika mjini kwake muda wa mchana hali akiwa ni mwenye kufuturu [hajafunga] basi haiwalazimikii kujizuia , bali yawalazimikia kulipa tu.
● Itajuzu kwa mwanamke kutumia dawa ambazo zitazuia jedhi kwa ajili ya funga au Hijja pale watakapotoa majibu wenye elimu za afya [madaktari] kuwa jambo hilo halitomletea madhara, *na iliyobora ni kujizuia na jambo hilo.*
Baaraka llaahu fiikum
________________________
✍️ Abuu Muyassam Alkujaaniy