
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 13, 2025 at 07:37 AM
*MUKHTASAR WA FUNGA:*
____________________
No.1️⃣0️⃣
*HUKMU MBALI MBALI ZA WAFUNGAJI:*
●Pindi atakapokula mwenye kufunga au akanywa au akafanya jimai kwa kusahau katika mchana wa Ramadhan basi funga yake ni sahihi wala hatopata dhambi.
•Na atakapolala akatokwa na manii ilihali amefunha basi funga yake ni sahihi na itamlazimu kukoga tu wala hatokuwa na dhambi; kwani yamemtoka bika khiyari yake kinyume na yule atakayejitoa manii kwa makusudi.
●Na atakayekuwa mgonjwa nanikawa kufunga kwake kunamtia shida na tabu kubwa na kunamletea madhara basi kufunga kwake ni haramu na kufuturu kwake ni wajibu, na atalipa baadae - ikiwa si katika ugonjwa ambao hautarajiwi kupona.
🔸️Na iliyobora kwa muislamu anatakikana adumu na tohara muda wote, na inajuzu kuchelewesha kukoga janaba au hedhi au nifasi mpaka kufika muda wa kuchomoza Alfajri ya pili, na funga ni sahihi. Lakini lililobora ni kujitoharisha kabla ya Alfajri.
🔸️Na anayetaka kusafiri hatotumia ruhusa za safari mpaka pale atakapoondokana na kuiacha mipanga ya mji wake - Na sunna kwa anayetaka kusafiri katika mwezi wa Ramadhan na akataka kufuturu basi asifuturu mpaka aiache mipaka ya mji wake.
🔸️Na itakapopaa ndege kabla ya kuzama jua na ikapanda juu zaidi angani, basi haimuhalalikii mfungaji kufuturu mpaka lizame jua.
🔸️Atakayekula kwa kuitakidi kuwa bado usiku kisha ikambainikia kuwa ni mchana, au akala kwa kuitakidi kuwa jua limezama kisha ikambanikia kuwa bado halijatua funga yake ni sahihi, wala haitomlazimu kulipa.
🔸️Na atakayefuturu kwa maslahi ya mwengine kama vile kufuturu kwa ajili ya kumuokoa mwenye kuzama, au mwenye kuungua moto na mfano wake basi ana ujira mkubwa, na itamlazimu kulipa tu na wala hana dhambi.
Baaraka llaahu fiikum
_____________________
✍️ Abuu Muyassam Alkujaaniy