MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 15, 2025 at 10:48 AM
*MUKHTASAR WA FUNGA:*
____________________
No.1️⃣1️⃣
*NAMNA YA KUFUNGA KATIKA MIJI AMBAYO JUA HALIZAMI:*
●Anayeishi katika miji ambayo jua halizami katika kipindi cha kiangazi wala halichomozi katika kipindi cha baridi, au katika miji ambayo nchana wake unaendelea miezi sita na usiku wake pia au zaidi na uchache wa hapo.
Yawapasa waswali na kufunga kwa kutegemea miji ya karibu na wao, watapambanua usiku kwa mchana, na itakuwa jumla ya usiku na mchana masaa ishirini na nne.
Wataseti mwanzo wa mwezi wa Ramadhani na mwisho wake, na kuanza kujizuia na kufuturu kwa kadri ya nyakati za huo mji wa karibu.
●Ambaye anaishi kwenye mji ambao unabainika mchana na usiku kwa kuchomoza jua na kuzama jua, hata kama utarefuka mmoja wao kwa kiasi kikubwa - basi ilivyo atafunga na kuswali kama aliyepo mji mwengine tu katika wakati ambao umepangiliwa kisheria.
Kwa mfano: Jua kwa kawaida huzama saa kumi na mbili na nusu jioni halafu ikawa linaongeza nusu saa kuzama kwake - hatutofungua mpaka lizame jua.
*HUKMU YA MWENYE KUACHA KUFUNGA RAMADHAN:*
●Mwenye kuacha kufunga Ramadhan hali ya kupinga uwajibu wake anakufuru.
●Mwenye kuacha kufunga Ramadhan kwa kuzembea tu na uvivu bila kupinga uwajibu wake hatokufuru na itasihi swala yake lakini atakuwa ni mwenye kupata dhambi kubwa kwa kuacha kwake nguzo kubwa katika nguzo za uislamu.
*HUKMU YA MWENYE KUSIKIA ADHANA NA CHOMBO [CHA KUNYWEA] KIPO MKONONI MWAKE:*
●Atakayesikia adhana ya Fajr ya pili na chombo kipo kwenye mkono wake, basi asikishushe mpaka akidhi haja yake.
Baaraka llaahu fiikum
_________________
✍️ Abuu Muyassam Alkujaaniy