MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 15, 2025 at 03:08 PM
🔸️ *KHATARI YA KUSWALI HARAKAHARAKA PASINA KUICHUNGA SWALA:* 🔸️
_________________
Amesema Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama:
*"KWA HAKIKA MTU ATASWALI MIAKA SITINI, NA HAITOKUBALIWA KWAKE SWALA [ HATA MOJA,] HWENDA ANATIMIZA RUKUU, NA HATIMIZI SIJDA, NA ANATIMIZA SIJDA NA WALA HATIMIZI RUKUU"*
________________
📚 Swahihu al Targhiib (529)
•••••••••••
*TAHADHARI:👌*
Tekeleza ibada ya swala kwa utaratibu sahihi pasina kuswali kwa haraka kwa namna ambayo unakosa kitulizano kwenye rukuu, sijda na kwenye kisimamo na kwenye kitako au hata kwenye kisomo.
Baaraka llaahu fiikum