MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 16, 2025 at 04:46 PM
*MUKHTASAR WA FUNGA:* _____________________ No. 1️⃣2️⃣ *● MAMBO YANAYOHARIBU FUNGA:* 1.Kula au kunywa kwa kukusudia wakati wa mchana wa Ramadhan. 2.Kufanya Jimani [tendo la ndoa] mchana wa Ramadhan Hili hutimia kwa kuzamisha kichwa cha uume kwenye tupu hata ikiwa haujatokwa na manii. 3.Kutoa manii hali ukiwa macho kwa njia ya kutomasana au kubusiana au kujichua [musterbation] au mfano wake katika mchana wa Ramadhan. 4.Kutumia dozi ya sindano inayotoa chakula kwa mwili katika mchana wa Ramadhan. 🤏 Na haya yanayoharibu funga mfungaji atakuwa ni mwenye kuiharibu funga yake pale atakapoyafanya kwa kukusudia, hali akiwa ni mwenye kujua hukmu yake akiwa ni mwenye kukumbuka. 5.Kutokwa na damu ye hedhi au nifasi mchana wa Ramadhan 6.Kuritadi [kutoka] katika dini ya uislamu -Allaah atukinge nalo. 📌 Ni haramu kumeza makohozi kwa mfungaji na asiyekuwa mfungaji, kwa sababu ni uchafu na yenye kuleta madhara kiafya - lakini hayaathiri funga [hayanguzishi]. Na ikiwa itajitokeza damu kwenye meno zake, au kwenye ulimi, au ameonja chakula basi asimeze, na pindi akimeza basi atakuwa ameharibu funga yake. *AMBAYO NI MAKRUHU KWA MFUNGAJI:* ●Ni karaha kwa mfungaji kuzidisha [kuyapeleka ndani zaidi] katika kusukutua na kuweka maji puani. ●Kuonja chakula bila haja. ●Kukusanya mate na kuyameza. ●Kufaya hijama na mfano wake... na kila ambacho ukikifanya kitakudhaifisha. 📍Mfungaji anawajibikiwa kujizuia na vyote vinavyoharibu funga kuanzia pale itakapomdhihirikia fajri ya kweli mpaka kuzama jua. Na ni wajibu kwake ajizuie na kujiweka mbali na kusengenya, kusema uongo, kutukana na mengineyo ndani ya Ramadhani na nje ya Ramadhan. Kwani yeyote ambaye hatoacha maneno ya uongo... basi Allaah hana haja na mfunga yake - wala hakuna haja yeye kuacha kula kwake na kunywa kwake..." Rejea: Bukhary [6057] Hii nii ishara kuwa mtu anatakiwa ajizuie na yote ya haramu isiwe ni sababu ya kuharibu funga yake pamoja na ibada zake zengine. Baaraka llaahu fiikum _________________________ ✍️ Abuu Muyassam Alkujaaniy
👍 1

Comments