MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 22, 2025 at 01:43 PM
*MUKHTASAR WA FUNGA:* ____________________ No.1️⃣3️⃣ *●HUKMU YA KUUNGANISHA FUNGA:* ☆Kuunganisha: yaani kufunga siku mbili na zaidi pasina kula wala kunywa. Kuunganisha kupo kwa namna mbili: 1.Kuunganisha mpaka wakati wa kula daku, yaani bila kula wakati wa kuanzia kuzama jua mpaka kufika usiku wa muda wa kula daku - jambo hili linajuzu, lakini linakuwa kinyume ya lile lililobora zaidi. 2.Kuunganisha mpaka kuzama kwa jua siku ya kesho yake - yaani akawa amekaa takriban masaa 48 kwa kukaa michana miwili na miusiku miwili na zaidi. Jambo hili ni lenye kukatazwa kisheria. Kwa ushahidi wa hadithi ya Abii Sa'eed Al khudriy katika swahihul Bukhary [1967] *●HUKMU YA MTU KUMBUSU NA KUGUSA NA KUMKUMBATIA MKEWE MCHANA WA RAMADHAN ILIHALI AMEFUNGA:* Hukmu ya kuwa karibu na mkeo na kumbusu, kumkumbatia na kumgusagusa [kumtomasa] kunafaa hata ikiwa matanio yake yatastuka kwa pale ambapo ataweza kuizuia na kuituliza nafsi yake, na pale atakapochelewa kutuka yale aliyoyaharamisha Allaah kunako kushuka kwa manii hapo inakuwa haramu yeye kufanya hivyo: Hivyo hapo tunapata funzo kuwa ikiwa hujiwezi kuzuia hisia zako za matamanio basi usijekujaribu kujiweka karibu na mkeo. *●HUKMU YA KUFANYA JIMAI [KUFANYA TENDO LA NDOA] KATIKA MCHANA WA RAMADHAN:* 1.Yatakapotoka manii jwa mfungaji kwa njia ya kujitoa manii [kujichua], au kwa kumtomasa mkewe pasina kufanya jimai basi atakuwa ni mwenye kupata dhambi na yamlazimu juu yake kufanya toba na kulipa siku aliyoiharibu pasina kafara. 2.Mwenyw kusafiri mwezi wa Ramadhan na akawa ni mwenye kufunga katika safari yake, kisha akamjamii mkewe katika mchana wa Ramadhan, basi atalazimikiwa na kulipa tu siku ile pasina kafara, wala hana dhambi; kwa sababu yeye ni msafiri, kadhalika ambao walisafiri [wanandoa] na hawakuwa ni wenye nia ya funga itaruhusika kwao. Wallaahu a’alaa wa a’alam Baaraka llaahu fiikum ___________________ ✍️ Abuu Muyassam Alkujaaniy

Comments