
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 23, 2025 at 02:59 PM
*NASAHA ZANGU KUHUSU KUISOMA QUR-AN;*
________________________
Ndugu zangu, kwanza nakuusieni tumcheni Allaah subhaanahu wata'aalaa kwa kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake.
QUR-AN: Kitabu cha Allaah kitukufu na maneno yake Allaah - alichoshushiwa Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama akiwa katika mji mtukufu wa Makka.
QUR-AN : imeshushwa ndani ya mwezi wa Ramadhan mwezi ambao upo karibu yetu apendapo Allaah.
Tunamuomba Allaah atuwafikishe kuufunga na kupata fadhla zake.
QUR-AN: Tunatakiwa tuisome na tusikie fahari kuyasoma maneno ya Allaah naye akitusikia - huku tukitarajia malipo makubwa tunapiisoma QUR-AN.
QUR-AN: Tuihifadhini, tuifanyie kazi na kuzingatia yaliyomo.
Haitoshi kwetu kuihifadhi tu pasina kufanyia kazi na kuzingatia yaliyomo. Bali baadhi ya watu wamejiwekea utaratibu kuwa wao ni kama vile mashabiki tu wakusubiria mashindano ya QUR-AN ima wadhamini au wakasikilize tu pasina wao kuisoma QUR-AN.
Tunachopaswa sote ni kuisoma QUR-AN wala tusisubirie muda fulani tu kuwa inapofika Ramadhani hadi Ramadhani - tuwe na mazoea ya kuisoma mara kwa mara kwani kuna fadhila mbali mbali za kuisoma QUR-AN wala usikate tamaa na kujiona wewe huwezi kuisoma na ukaona ni baadhi ya watu tu ndio wao ndio watasoma wewe ukajiweka fungu la kusikiliza tu.
Yeyote atakayefanya amali yoyote ile ni kwa ajili ya nafsi yake.
Aidha, kwa wale walioihifadhi QUR-AN watumie fursa ya kujua tafsir ya QUR-AN na kuhifadhi hadithi za Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama wajibweteke kuona wamehifadhi tu lakini hawajui maana ya kile walichokihifadhi na kufikia lengo lake ambalo ni kuifanyia kazi.
Vile vile wanaosoma na kuihifadhi QUR-AN wawe na athari ya QUR-AN isiwe mwenye kuihifadhi QUR-AN amegubikwa na kila laghwu na lahwu na kila tabia chafu.
Mwenye kuihifadhi QUR-AN awe kigezo chema katika mienendo na akhlaq nzuri ajipambe kwa tabia njema za kiislamu.
Yote kwa yote : tuisomeni QUR-AN kwa jili ya kutekeleza maamrisho ya sheria na kumfanyia Allaah pekee ibada hii na sio kwa kujionesha [kutaka watu wakuone] au kutaka watu wakusikie kuwa una sauti nzuri au umejifadhi sana au kwa kuhitajia jambo fulani.
Pongezi kwa walezi na waalimu
❤️
👍
2