MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 24, 2025 at 09:32 AM
*MUKHTASAR WA FUNGA:* ___________________ No. 1️⃣4️⃣ *HUKMU YA MWENYE KUFANYA JIMAI KATIKA MCHANA WA RAMADHANI:* ●Atakayefanya jimai katika mchana wa Ramadhan hali akiwa ni mkazi - yaani si msafiri - mwenye kukusudia, mwenye kujua na aliyekumbuka basi atakuwa ni mwenye kupata dhambi, na itamlazimu kuleta toba na talipa na atatoa Kafara. Ama akiwa ni mwenye kulazimishwa, au hajui hukmu, au aliyesahau basi funga yake ni sahihi wala hatopata dhambi kwa hilo wala hatolipa wala hatokuwa na kafara na mwanamke ni kama mwanaume kwenye hukmu hiyo. ●Ikiwa atamuingilia mkewe siku mbili au zaidi katika mchana wa Ramadhan itamlazimu kafara na kulipa kwa idadi ta siku, na ikiwa atakariri ndani ya siku moja - yaani atalifanya tendo hilo mara zaidi ya moja kwa mchana mmoja - basi kafara yake ni moja pamoja na kulipa. ●Atakaporudi safarialiyesafiri akafika kwake katika mchana wa Ramadhan na kumkuta mkewe ametoharika kutokana na hedhi au nifasi katika muda huo itajuzu kwake kumuingilia. *✂️ KAFARA YA KUFANYA JIMAI KATIKA MCHANA WA RAMADHANI:* ✔️Kuacha mtumwa huru, ikiwa hakupata, basi atafunga miezi miwili mfululizo, ikiwa hawezi atalisha masikini sitini kila maskini mmoja nusu pishi ya chakula ikiwa hatopata basi hudondoka kafara. Na kafara haiwajibiki isipokuwa kwa kufanya jimai katika mchana wa Ramadhan kwa yule ambaye inamlazimu kufunga pale atakapofanya jambo hilo hali akiwa ni mwenye kujua na kwa kukusudia na kukumbuka. 🤏Wala hakuna kafara kwa yule ambaye atafanya tendo hilo katika funga ya sunna, au nadhri au fuga ya kulipa, au akiwa kwenye safari. *●MAMBO AMBAYO HAYAKATI MFULULIZO WA UFUNGAJI KWA MWENYE KAFARA YA KUFUNGA MIEZI MIWILI MFULULIZO:* Mambo amabayo hayakati mfululizo huoni kama vile: a).Eid mbili - na hapa inaingia Eid ya kuchinja kwa sababu ya Fitr inatanguliwa na Ramadhan ambayo hakuna kulipa deni ndani yake. b).Safari c).Maradhi ambayo yanayoruhusika mtu kufuturu. d). Hedhi na nifasi. Baaraka llaahu fiikum _____________ ✍️Abuu Muyassam Alkujaaniy

Comments