
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 25, 2025 at 08:57 AM
*MUKHTASAR WA FUNGA:*
__________________
No. 1️⃣6️⃣
*SUNNA ZA FUNGA:*
1.Inasuniwa kwa mwenye kufunga ale daku; kwa sababu kula daku kuna baraka, na ni sunna kuichelewesha mpaka kukaribia na adhana ya fajr, na bora ya daku ya muislamu ni tende.
Na katika baraka za daku ni kupata nguvu katika kumtii Allaah na kumfanyia ibada, nayo ni sababu ya kusimama usiku wakati wa thuluthi ya mwisho ya usiku wakati wa kuomba istighfaar na dua, na kuswali swala ya fajri kwa jamaa na kuwakhaifu mayahudi na manaswara.
2.Inasuniwa kuwahi kufuturu, na iwe kwa tende kabla ya kuswali, ikikosekana tende basi japo kwa maji, akikosa basi kwa chakula chochote kitakachokuwa chepei kwake au kinywaji cha halali, ama akikosa vyote atanuia tu moyoni mwake kufuturu.
Na kufuturu kwa tende ni ibada na chakula, na tamu, na tunda na dawa.
3.Inasuniwa kwa mwenye uwezo kuwafuturisha wafungaji; kwa kile kinachopatikana kunako kuwafanyia ihsani masikini, na kuingiza upendo, na kupata malipo makubwa.
4.Inasuniwa kwa mfungaji akithirishe kumtaja Allaah na kuomba dua, kusoma Qur-an, na inasuniwa akishafuturu aseme : _"Dhahaba al dhwamau, wabtallatil 'uruuqu, wathabatal ajru in shaa Allaahu"_
5.Inasuniwa kwa mwenye kufunga na asiyekuwa mwenye kufunga kupiga mswaki wakati wote.
6.Inasuniwa kwa mfungaji pale ikitokea kuna mtu amemtukana au kugombana naye aseme: _"Mimi nimefunga, mimi nimefunga"_
7.Inasuniwa kwa mwenye kufunga kukithirisha na kuzidisha kunako matendo ya kheri, kama vile dhikri, kusoma Qur-an, kuamrisha mema, kukataxa maovu, kutoa swadaqa, istighfaar na kuleta toba, kusimama usiku, kuunga udugu, kuwatembelea wagonjwa na mfano wake.
8.Inasuniwa swala ya taraweh katika kila usiku wa Ramadhan baada ya swala ya isha (Rakaa kumi na moja pamoja na witri au rakaa kumi na tatu pamoja na witri) hiyo ndio sunna na atakayezidisha hakuna ubaya wala karaha. Na atakayeswali pamoja na imamu mpaka akamaliza huandikiwa thawabu za kisimamo cha usiku.
9.Inasuniwa kwa atakayeitwa /kukaribishwa chakula mchana hali akiwa ni mwenye kufunga aseme: _"Mimi nimefunga"_
10.Inasuniwa kutekeleza 'Umra katika mwezi wa Ramadhan, na kujibidiisha kwa ibada katika masiku kumi ÿa mwisho.
_______✍️