
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 26, 2025 at 10:54 AM
*MUKHTASAR WA FUNGA*
___________________
No. 1️⃣7️⃣
*NYAKATI BORA ZAIDI ZA KISHERIA:*
●Mwezi wa Ramadhan ndio mwezi mtukufu zaidi kuliko miezi yote. Na usiku wake katika masiku kumi ya mwisho ndio bora zaidi kuliko mchana wa masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Dhulhijja. Kwa sababu ndani ya masiku hayo ya Ramadhan kuna usiku wa Laylatul qadr.
●Na mchana wa masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Dhulhijja ni bora zaidi kuliko mchana wa masiku kumi ya mwisho ya mwezi wa Ramadhan, kwa sababu ndani ya masiku ya mwazo wa mwez wa Dhulhijja kuna ndani yake siku ya kuchinja (10 Dhulhijja) na siku ya 'Arafa.
●Na siku ya Al juma'a ndiyo siku bora ya wiki (ndiyo siku kuu ya wiki), na siku ya kuchinja ndiyo siku bora ya mwaka, na usiku wa laylatul qadr ndio usiku bora zaidi wa mwaka.
*🔸️FADHILA ZA LAYLATUL QADR:*
●Laylatul qadr ni usiku wenye utukufu mkubwa, ndani yake hupambauliwa na kubainishwa kila jambo la hekma, na hukadiriwa riziki na hatima ya kila jambo na kila hali kwa ajili ya mwaka huo.
●Na unatarajiwa kupatikana usiku huu katika masiku ya witri katika kumi la mwisho yaani usiku wa mwezi 21, 23, 25, 25 au 29 na wenye kupewa kiapo mbele zaidi ni usiku wa mwezi 27.
Na kwa hakika Allaah ameuficha usiku wa laylatul qadr kama alivyoificha sa'atul ijaaba katika siku ya Al juma'a; kwa ajili watu wajitahidi katika kufanya ibada kwa wingi, na wajivunie ujira mkubwa kutoka kwa mola wao.
●Laylatul qadr fadhla zake ni bora kuliko miezi elfu moja, nayo ni miaka 83 na miezi minne, nayo hiyo ni katika mambo ya kiupekee katika umma huu, ni sunna kuuhuwisha usiku huo kwa kufanya ibada, na kukithirisha dhikri na istighfaar, na kukithirisha dua katika zile zilizothibiti.
🤏 Dua ya kuomba kwa atakayeafikishwa kuupata usiku huo aombe kwa kusema: _"Allaahumma innaka 'afuwwun, tuhibbul 'afwa fa'afu 'annii"_
Baaraka llaahu fiikum
____________________
✍️ Abuu Muyassam Alkujaaniy