MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 28, 2025 at 02:48 PM
*MUKHTASAR WA FUNGA* ________________ No. 1️⃣8️⃣ *FUNGA YA SUNNA:* _NAMNA YA FUNGA YA MTUME swalla llaahu 'alayhi wasallama na KUFUTURU KWAKE_ 🤏 HADITHI ya Ibnu 'Abbaas _radhwiya llaahu 'anhuma_ iliyopo katika swahihayni inalifafanua hilo kuwa: Hakupatapo Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama kufunga mwezi kamili isipokuwa Ramadhan, na alikuwa akifunga mpaka husema msemaji hatofungua, na alikuwa anabakia hafungi mpaka husema msemaji kuwa hatofunga. *●UTARATIBU WA MTUME _swalla llaahu 'alayhi wasallama_ KATIKA FUNGA YA SUNNA:* Funga ya Mtume _swalla llaahu 'alayhi wasallama_ katika kufunga sunna kunagawanyika katika aina tatu: 1.Zile alizopendelea kufunga na kudumu nazo kama vile kufunga siku tatu katika kila mwezi, na mwezi kumi katika mwezi wa Muharram 2.Alizopendelea kufunga na akakithirisha kwake kufunga kama vile funga ya Sha'aban 3.Alizopendelea kufunga lakini haikunukuliwa kwake kufunga, na hivyo hwenda ni kwa kushughulishwa kwake na udhuru - au hwenda alifunga lakini haikunukuliwa tu. Kama vile kufunga sita za Shawwal, na kufunga siku moja na kuacha moja [funga ya Daūd] Na lile lililo la wajibu kwetu ni kumtii Mtume swalla llaahu 'alayhi wasallama, na kufanya vizuri katika kumfata katika kauli zake na matendo yake na akhlaqi zake; kwani yeye ndiye kigezo chema kwetu. Rejea Qur-an 33: 21 [Al ahzaab] *VIGAWANYO VYA FUNGA YA KISHERIA:* Funga ya kisheria ipo ya aina mbili: *1.Funga ya wajibu:* mfano funga ya Ramadhan, funga ya Nadhri, funga ya kafara ya yamini, na kuua kwa makosa, dhwihar, na kuharibu funga kwa kufanya jimai mchana wa Ramadhan. *2.Funga ya sunna:* nayo ipo ya aina mbili: a). Sunna zilizoachiliwa. (b).Zilizofungamanishwa na wakati maalum, na baadhi yake zipo zilizotiliwa mkazo/msisitizo zaidi dhidi ya nyengine. Funga za sunna ndani yake kuna thawabu kubwa, na kuzidishiwa katika ujira, pale atakapoitakasa mfungaji funga yake kwa kuepusha na yale yote yasiyomridhisha Allaah. Baaraka llaahu fiikum ______ Abuu Muyassam Alkujaaniy✍️______

Comments