MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 28, 2025 at 03:33 PM
*MUKHTASAR WA FUNGA:* ___________________ No. 1️⃣9️⃣ *AINA ZA FUNGA ZA SUNNA:* Funga za sunna zipo za aina nne: 1. Zile zenye kujikariri kwa kujikariri kwa siku, kama vile funga siku moja na kufuturu nyengine. 2.Zenye kujikariri kwa wiki, kama vile funga ya Jumatatu na Alhamisi 3.Zenye kujikariri kwa miezi, kama vile kufunga siku tatu katika kila mwezi. 4.Zenye kujikariri kwa miaka, kama vile kufunga siku ya 'Arafa, na mwezi kumi Muharram ['Aashuraa], na sita za Shawwal *VIGAWANYO VYA FUNGA ZA SUNNA:* Zinagawanyika funga za sunna katika vigawanyo nane, nazo: *Kwanza:* funga ya sunna iliyobora zaidi ni funga ya Daūd (kufunga siku moja ukaacha moja). *Pili:* Funga iliyobora baada ya Ramadhan ni mwezi wa Muharram - na iliyotiliwa msisitizo zaidi ni mwezi kumi , kisha tisa, na funga ya mwezi kumi inafuta makosa ya mwaka uliopita , na inasuniwa kufunga tisa kisha kumi kuwakhalifu mayahudi. *Tatu:* Funga ya sita za Shawwal - ubora wake kwa aliyefunga Ramadhan na kuunganisha sita ni kama aliyefunga mwaka mzima. Na iliyobora ni kufunga kwa kufatiliza baada tu ya 'Eid na inajuzu kuitofautisha. Ama kwa yule ambaye ana deninla Ramadhan anatakiwa kulipa kwanza Ramadhan kisha afunge sita. *Nne:* Kufunga siku tatu katika kila mwezi, nazo kwa ubora ni kama kufunga mwaka mzima, na inasuniwa kuwa katika masiku meupe nayo ni 13, 14 na 15 na akipenda anaweza kufunga mwanzoni au mwishoni mwa mwezi. *Tano:* Kufunga siku tisa za mwanzo wa mwezi wa Dhulhijja, na iliyobora zaidi ni siku ya tisa ambayo ni siku ya 'Arafa kwa aiyekuwa Hajj (aliyepo kwenye hijja). Na funga yake inafuta madhambi ya mwaka uliopita na ujao. *Sita:* Kufunga katika njia ya Allaah *Saba:* Inapendelewa kukithirisha kufunga katika mwezi wa sha'aban kuanzia mwanzo wake na sio kuanza kati kati yake au mwishoni. *Nane:* Kufunga siku ya Jumatatu na Alhamis katika kila wiki. ●Inapendezwa kwa msafiri kufunga siku ya 'Arafa, na mwezi kumi Muharram ili adiriki thawabu zake, kwa sababu muda wake unampita. Baaraka llaahu fiikum _______________________ ✍️Abuu Muyassam Alkujaaniy

Comments