MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
February 28, 2025 at 08:47 PM
🤏 *TANBIIH* ******** 1. *TUNAOSWALISHA WATU TARAWEH TUSIWANYIME WATU FADHLA ZA KUSWALI RAATIBA [RAKAA MBILI ZA BAADIA] BAADA YA SWALA YA ISHA* _Unakuta baadhi yetu baada tu ya adhkaar au wengi hata bila adhkaar husimama kuswalisha taraweh._ 2. *TUSIKIMBIE SPIIDI KWENYE KUSWALISHA MPAKA IKAWA HAKUNA TUMAANINA KWENYE SWALA - HAIJULIKANI RUKUU WALA SIJDA* _Swala ya taraweh haijahusishwa na kuswaliwa kwa spiid, swala zote ziwe za faradhi au sunna lazima utekeleze nguzo zake na sharti zake_ 3. *MAAMUMA USISUBIRIE MAKUSUDI MPAKA IMAMU ANAMALIZA KISOMO NDIO UNAENDA KUUNGA SWALA KWENYE RUKUU ILIHALI UPO HAPO HAPO, UKAACHA KUSOMA SUURATUL FAATIHA - HAPO UTAKUWA UMEACHA NGUZO KWA KUKUSUDIA NAWE SIO MASBUUQ ITAKUWA UMEHARIBU SWALA* _Wallaahu a’alaa wa a’alam_ Baaraka llaahu fiikum

Comments