Duro Crypto
Duro Crypto
February 2, 2025 at 02:24 PM
*Mtaji wa Soko la Crypto ni Nini?* Mtaji wa soko (market cap) unapatikana kwa kuzidisha idadi ya sarafu zinazozunguka (circulating supply) na bei ya sarafu moja. Mfano: Tuseme tuna miradi miwili ya crypto: AliceCoin na BobCoin. AliceCoin ina jumla ya sarafu 1,000, na zote zipo kwenye mzunguko. BobCoin ina jumla ya sarafu 100,000, lakini ni 60,000 tu zipo kwenye mzunguko. Bei ya AliceCoin ni $100, wakati BobCoin ni $2. Tukihesabu mtaji wa soko: AliceCoin: 1,000 × $100 = $100,000 BobCoin: 60,000 × $2 = $120,000 Japokuwa bei ya AliceCoin ni kubwa kuliko BobCoin, bado BobCoin ina thamani kubwa zaidi sokoni kwa sababu ina sarafu nyingi zaidi kwenye mzunguko. Kwa hiyo, thamani ya sarafu moja haitoshi kuelezea thamani ya mtandao wa cryptocurrency; market cap ndiyo kipimo bora zaidi.

Comments