
Duro Crypto
400 subscribers
About Duro Crypto
Crypto Educator | Blockchain Simplifier | Bitcoin for All | Navigating Crypto Dips | Vision for 2025: Crypto as Easy as Banking
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Seneti ya Marekani imepitisha rasmi hatua ya kuendelea kujadili mswada wa sheria wa 'GENIUS Act' unaohusu stablecoin Warren matopeni😃haelewi amevurugwa


*Faida na Hasara za Kuwekeza kwenye Crypto* *Faida:* Inafikika kirahisi: Mtu yeyote mwenye intaneti anaweza kutumia. Imejitegemea (decentralized): Haina mamlaka ya kati, hivyo ni vigumu kuidhibiti au kuizuia. Inaweza kupambana na mfumuko wa bei: Hazitegemei sera za mabenki ya kati. Njia nyingi za kupata faida: Mbali na kuuza na kununua, unaweza kuwekeza kwa staking, liquidity, nk. Ina matumizi ya ziada: Baadhi ya tokeni zinatoa faida ya kipekee kama kushiriki maamuzi ya miradi au kupata ofa kutoka kwa timu za michezo unazozipenda. *Hasara:* Bei hubadilika ghafla: Inaweza kupanda au kushuka sana kwa muda mfupi. Utaratibu wa kisheria bado haujakaa sawa: Kila nchi ina sheria zake kuhusu crypto. Hatari ya kupoteza wallet: Ukisahau neno siri au ukipoteza wallet yako ya kidigitali, unaweza kupoteza pesa zako zote. Faida si ya uhakika: Kama soko lolote la kifedha, hakuna uhakika wa kupata faida kila wakati. *Faida na Hasara za Kuwekeza kwenye Hisa* *Faida:* Zinapatikana kwa urahisi zaidi siku hizi: Kuna apps na tovuti nyingi zinazokuwezesha kuwekeza kwa urahisi. Zinadhibitiwa na serikali: Kuna taasisi kama CMSA zinazosimamia masoko ya hisa kulinda wawekezaji. Uchaguzi ni mpana: Unaweza kuchagua hisa kulingana na sekta, kampuni, na hata kama zinalipa gawio au la. *Hasara:* Bei hubadilika pia: Kama kampuni inafanya vibaya au ikipata habari mbaya, thamani ya hisa inaweza kushuka. Gharama za juu: Mara nyingi, kununua au kuuza hisa huambatana na ada kubwa kuliko crypto. Hakuna uhakika wa faida: Kama ilivyo kwa crypto, hakuna mtu anayehakikishiwa faida kila mara. *Hitimisho* Ingawa crypto na hisa ni vitu tofauti, vyote vinaweza kutumika kama njia ya kuwekeza. Cha msingi ni kujua faida na hatari zake, na kufanya utafiti wako (Do Your Own Research - DYOR) kabla ya kuwekeza. Wekeza kwa akili na usiweke pesa zako zote sehemu moja.

1. Bitcoin imevuka dola 100,000 na watu wakubwa wanaendelea kuinunua, wakitarajia bei itaendelea kupanda. 2. Coinbase ilishambuliwa na hackers, lakini hisa zake zimepanda asilimia 24 baada ya kuingizwa kwenye orodha ya makampuni makubwa Marekani. 3. Watu wa crypto Ufaransa wanahofia utekaji baada ya matukio ya watu kutekwa na kutishiwa. 4. Ethereum na Solana zimepanda bei kwa kasi, huku XRP ikitabiliwa makubwa kufikia dola 250 mwaka 2026. 5. Sheria mpya ya stablecoins Marekani imesimama, kutokana na wasiwasi juu ya familia ya Trump kuhusika na biashara za crypto.


Bei ya Bitcoin imefikia rekodi mpya ya juu kabisa, sasa inauzwa kwa dola 109,424.


Hapa bado *Mr too late* haja cut interest rate , akija kupunguza interest rate,nadhani ni juu mawinguni😀

*Crypto vs Hisa: Kuna Tofauti Gani?* *Cryptocurrency* ni nini? Cryptocurrency ni pesa za kidigitali ambazo zinatumia teknolojia ya blockchain kuhakikisha miamala ni salama na ya kuaminika. Zinaweza kutumika kama njia ya kulipia au kuhifadhi thamani. Zinapatikana mtandaoni na hazihitaji benki wala taasisi ya kati kuziendesha. Thamani yake inategemea uhitaji na upatikanaji wake sokoni. *Hisa ni nini?* Hisa ni umiliki wa sehemu ya kampuni. Ukimiliki hisa, ni kama unamiliki kipande kidogo cha kampuni hiyo. Faida ya kampuni ikiongezeka, unaweza kupata gawio (dividendi). Thamani ya hisa hubadilika kulingana na utendaji wa kampuni na habari mbalimbali kuhusu kampuni hiyo. *Tofauti Kuu Kati ya Crypto na Hisa* Ukiwekeza kwenye crypto, hupati umiliki wa kampuni kama ilivyo kwenye hisa. Crypto haikulipi gawio, ila unaweza kuitumia kupata kipato kwa njia kama staking au yield farming. Crypto inapatikana saa yoyote, usiku na mchana, kupitia crypto exchanges. Lakini hisa huuzwa kwenye masoko rasmi ya hisa ambayo yana muda maalum wa kufunguliwa. Crypto ni teknolojia mpya sana ikilinganishwa na hisa ambazo zimekuwepo kwa miongo mingi. *Je, Niwekeze Wapi, Crypto au Hisa?* Zote zina faida na changamoto zake. Uamuzi unategemea uvumilivu wako wa hatari (risk tolerance), malengo yako, na muda unaotaka kusubiri kabla ya kuona faida. Wekeza kwa busara na usiweke pesa yote sehemu moja unaweza kuzigawanya kwenye crypto na kwenye hisa.
