
Duro Crypto
February 2, 2025 at 02:38 PM
*Kwa Nini Mtaji wa Jumla wa Soko la Crypto Unaweza Kuwa wa Kupotosha?*
Kufanya maamuzi ya kifedha kwa kuzingatia tu total crypto market capitalization kunaweza kuwa na changamoto na upotoshaji kwa sababu kadhaa:
1. Tatizo la Taarifa Sahihi za Usambazaji wa Sarafu
Ili kupata market cap sahihi, tunahitaji kujua idadi halisi ya sarafu zinazozunguka (circulating supply).
Ikiwa data hii ni mbaya au haipo sahihi, hesabu yoyote inayofanywa juu yake itakuwa batili.
2. Uwezekano wa Kudanganya Soko
Baadhi ya miradi ya crypto inaweza kudanganya au kupandisha thamani ya soko kimakusudi ili kuwahadaa wawekezaji kwamba wana thamani kubwa zaidi kuliko ilivyo kweli.
Hii inaweza kuwafanya watu wawekeze kwa kuamini kuwa mradi una nguvu kubwa, ilhali ni hadaa.
3. Thamani Inayobadilika Kwa Haraka
Market cap ni picha ya soko kwa muda fulani—yaani, ni thamani inayoweza kubadilika kwa siku, wiki, au hata masaa machache.
Leo inaweza kuwa na thamani ya trilioni 1, wiki ijayo bilioni 500, na miezi sita baadaye milioni 900.
Kutegemea namba hii pekee bila kuchunguza undani wa soko kunaweza kuwa na madhara kwa wawekezaji.
🙏
1