Duro Crypto
February 6, 2025 at 03:40 AM
*🔴 HABARI MPYA: ELON MUSK AUNGA MKONO MATUMIZI YA BLOCKCHAIN KWA MALIPO YA SERIKALI YA MAREKANI!*
Elon Musk, mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Serikali ya Marekani, amesema anaunga mkono mpango wa kutumia blockchain kuhifadhi na kufuatilia malipo ya serikali ya Marekani.
Kupitia mtandao wa X, Musk alisema maafisa wa Hazina ya Marekani wamekuwa wakikiuka sheria kwa kuidhinisha malipo yasiyo halali kila siku. Akaongeza kuwa hali hii lazima ikomeshwe mara moja!
Ripoti zinasema kuwa serikali ya Trump tayari imeanza kuchunguza jinsi teknolojia ya blockchain inaweza kusaidia kupunguza gharama, kufuatilia matumizi ya fedha za serikali, na hata kusaidia kulipa madeni.
Bado haijulikani kama Musk atatumia blockchain maarufu kama Bitcoin, Ethereum, Dogecoin, au kama ataunda mfumo mpya kabisa kwa ajili ya serikali.