
Duro Crypto
February 9, 2025 at 07:35 AM
*Je, Nifanye Biashara au Niwekeze?*
Kabla hujanunua crypto, jiulize kama unataka kuwa mwekezaji au mfanyabiashara (trader). Ingawa maneno haya mawili mara nyingi hutumika kwa kubadilishana, yana maana tofauti:
Uwekezaji: Hapa unanunua crypto na kuishikilia kwa muda mrefu, ukiamini kuwa thamani yake itaongezeka kwa miaka ijayo. Hii inahitaji subira na siyo lazima ufatilie soko kila mara.
Biashara ya Crypto (Trading): Hapa unanunua na kuuza crypto mara kwa mara ili kupata faida ya muda mfupi au wa kati. Trading inahitaji muda mwingi, maarifa ya kina, na mkakati mzuri. Pia, gharama za miamala zinaweza kuwa kubwa.
Masoko ya crypto yana mabadiliko makubwa ya bei (volatility). Ingawa traders wanatumia volatility kupata faida, inaweza pia kuleta hasara kubwa.
Kwa wanaoanza, uwekezaji wa muda mrefu ni njia rahisi na salama zaidi. Wawekezaji wanaangalia zaidi uimara wa mradi badala ya mabadiliko ya bei za muda mfupi.
Baadhi ya watu wanapendelea kuwekeza tu, wengine wanafanya trading pekee, na baadhi wanachanganya vyote viwili. Chochote unachochagua, hakikisha huwekezi pesa ambazo huwezi kumudu kupoteza.
Ikiwa unataka kujifunza zaidi kuhusu day trading na swing trading,basi endelea kuwa na subira,tutazungumzia siku zijazo topic za mbeleni
🔥
1