
Duro Crypto
February 9, 2025 at 07:40 AM
*Uchambuzi wa Msingi vs. Uchambuzi wa Kiufundi*
Kabla ya kuwekeza, unahitaji kuchambua sarafu ili kujua kama ni chaguo zuri. Kuna aina mbili kuu za uchambuzi:
*1. Uchambuzi wa Msingi (Fundamental Analysis - FA)*
Hii inahusisha kuchunguza uimara wa mradi mzima, ikiwa ni pamoja na matumizi ya sarafu hiyo, timu inayoiendesha, nyaraka zake (whitepaper), maendeleo ya kiteknolojia, masoko yake, usimamizi wake, na malengo yake ya muda mrefu.
*2. Uchambuzi wa Kiufundi (Technical Analysis - TA)*
Hii inahusisha kuchambua mwenendo wa bei za nyuma ili kutabiri mwelekeo wa bei zijazo. Hutumia chati za mishumaa (candlestick charts) na viashiria mbalimbali kama wastani wa bei za nyuma (moving averages) na mistari ya mwenendo (trend lines).
Kama unafanya uwekezaji wa muda mrefu, hutahitaji kufuatilia mabadiliko ya bei kila siku. Hata hivyo, kama unafanya trading, uchambuzi wa kiufundi ni muhimu ili kuelewa mwelekeo wa soko na kufanya maamuzi bora.
❤️
🔥
🥳
3