Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
February 9, 2025 at 02:09 PM
*KIGOMA BROTHERS* *LEO KTK HISTORY* Hawa ni vijana watanashati kutoka mkoani kigoma Ujiji Enzi hizo. Wazee wetu wameanza Harakati za kuupambania mkoa wetu Kigoma kabla ya uhuru na kusaidia Jamii Yao ya kigoma. Wanayohistori yenye kutukuka ndani ya mkoa wetu Umoja wao huo wa *KIGOMA BROTHERS* waliuunda Mahususwi kwa Ajili ya kuwasaidia ndugu zao Wakigoma waliopo Dar es salaam wanapofikwa na matatizo,magonjwa n.k..wao hujitoa na kuwasaidia bila ya Ujira wowote. Hii ilionesha kujali na kuthamini Jamii Yao ya watu Wakigoma na kujitoa kwa Moyo wao mkunjufu. Nahii waliifanya kwa bila Kubagua huyu anatoka Wilaya ipi ktk mkoa Wakigoma. Walikua na Upendo sana wazee wetu Enzi hizo. Kwa kuthamini mchango wao ,utu na undugu kwa watu Wakigoma na tawataja kwa majina Yao kama Ilivyoripotiwa kutoka kwenye makitaba ya Jamii ya watu Wakigoma kutoka mji mkongwe wa UJIJI. *Kuanzia Kushoto waliosimama* Marehem Mzee Aman Fukuza. Marehem Mzee Idd Ally Lubumba. Marehem Mzee Abdulbari, na Marehem Mzee Ally Juma Lhey. *Walioketi kutoka Kushoto* Marehem Mzee Rajab Kitete Marehem Mzee Omar Fukuza Marehem Mzee Abdallah Fundi Mwamba na Marehem Mzee Juma Rangam. Mungu awalipe Kila lakheri na awaondolee Adhabu ya akaburi. Picha hii imepigwa Tarehe 05/04/1951 wazee wetu wamenyuka pamba safi na watanashati haswaa *#kigoma ya Upendo* *#kigoma yetu* Tuwape Mauwa Yao 🌹🌹🌹🌹🌹 https://whatsapp.com/channel/0029VabqKek7oQhlIA20XA2P
👍 😢 😮 3

Comments