Kigoma Region Tanzania WhatsApp Channel

Kigoma Region Tanzania

242 subscribers

About Kigoma Region Tanzania

Jumuiya ya Watu wa Kigoma (Kigoma People's Community) Lengo kuu ni kuwaleta wanakigoma pamoja kama familia moja yenye lengo moja la kusaidia kuharakisha maendeleo ya Mkoa wetu wa Kigoma kuanzia mtu mmoja mmoja hadi makundi ya watu. Hii ni Jumuiya ambayo inawaleta watu wote pamoja bila kujali maeneo yao, kabila zao, dini zao, hali zao za kiuchumi wala utashi wao wa kisiasa. Mjumuiko huu unafanya kazi kwa lengo la kuleta Nguvu kwa pamoja katika kuendeleza na kuharakisha maendeleo ya Mkoa wa Kigoma. Jumuiya ina malengo mengi na mikakati mingi itakayo tuhusu sisi kama wanafamilia. Tutawajibika pia katika matukio ya kudhibiti ujinga, maradhi, umasikini, kuinua uchumi, Elimu, Vipaji, Fursa, Ajira, Kushiriki Habari na matukio, Haki na Usawa kwa watu wa mkoa wa Kigoma. Tunasimama kama kielelezo chema cha kuutangaza mkoa wetu ndani na nje ya mipaka ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jumuiya ya Watu wa Kigoma inafanya kazi nchi nzima na inamuhusu Mwanakigoma yeyote yule popote pale alipo.

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
2/9/2025, 2:09:50 PM

*KIGOMA BROTHERS* *LEO KTK HISTORY* Hawa ni vijana watanashati kutoka mkoani kigoma Ujiji Enzi hizo. Wazee wetu wameanza Harakati za kuupambania mkoa wetu Kigoma kabla ya uhuru na kusaidia Jamii Yao ya kigoma. Wanayohistori yenye kutukuka ndani ya mkoa wetu Umoja wao huo wa *KIGOMA BROTHERS* waliuunda Mahususwi kwa Ajili ya kuwasaidia ndugu zao Wakigoma waliopo Dar es salaam wanapofikwa na matatizo,magonjwa n.k..wao hujitoa na kuwasaidia bila ya Ujira wowote. Hii ilionesha kujali na kuthamini Jamii Yao ya watu Wakigoma na kujitoa kwa Moyo wao mkunjufu. Nahii waliifanya kwa bila Kubagua huyu anatoka Wilaya ipi ktk mkoa Wakigoma. Walikua na Upendo sana wazee wetu Enzi hizo. Kwa kuthamini mchango wao ,utu na undugu kwa watu Wakigoma na tawataja kwa majina Yao kama Ilivyoripotiwa kutoka kwenye makitaba ya Jamii ya watu Wakigoma kutoka mji mkongwe wa UJIJI. *Kuanzia Kushoto waliosimama* Marehem Mzee Aman Fukuza. Marehem Mzee Idd Ally Lubumba. Marehem Mzee Abdulbari, na Marehem Mzee Ally Juma Lhey. *Walioketi kutoka Kushoto* Marehem Mzee Rajab Kitete Marehem Mzee Omar Fukuza Marehem Mzee Abdallah Fundi Mwamba na Marehem Mzee Juma Rangam. Mungu awalipe Kila lakheri na awaondolee Adhabu ya akaburi. Picha hii imepigwa Tarehe 05/04/1951 wazee wetu wamenyuka pamba safi na watanashati haswaa *#kigoma ya Upendo* *#Kigoma yetu* Tuwape Mauwa Yao ๐ŸŒน๐ŸŒน๐ŸŒน๐ŸŒน๐ŸŒน https://whatsapp.com/channel/0029VabqKek7oQhlIA20XA2P

๐Ÿ‘ ๐Ÿ˜ข ๐Ÿ˜ฎ 3
Image
Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
2/11/2025, 2:15:59 PM

*USAFIRI NDANI YA MTO MALAGARASI -KIGOMA* *#UTALII WA NDANI* *#UTALII KIGOMA* https://whatsapp.com/channel/0029VabqKek7oQhlIA20XA2P

Image
Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
2/14/2025, 3:59:34 PM

*UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMAENDELEO MKOANI* Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia, mkoa wa Kigoma umepokea Shilingi Trilioni. 11.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo huku baadhi ya miradi utekelezaji wake umekamilika na ambayo haijakamilika ipo katika hatua za utekelezaji na hakuna mradi uliokwama. Masuala yote ya ujenzi yanasimamiwa na kanuni na Sheria zinazotokana na mikataba hivyo mkandarasi anapotakiwa kuongeza muda wa utekelezaji mradi, serikali itahakikisha nyongeza ya muda huo itakuwa ni ile inayokidhi matakwa ya kimkataba. Niwahakikishie kuwa miradi ya TACTIC inayoendelea kutekelezwa mkoani Kigoma itakamilika kwa mujibu wa mikataba yake sambamba na miradi yote inayotekelezwa mkoani hapa" Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye

Image
Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
2/16/2025, 8:40:37 PM

*MALENGO YETU KIGOMA COMMUNITY NA KIGOMA REGION TANZA* Hii ndio kazi inayotakiwa kuanza kuifanya *Jamii ya watu wakigoma* Mungu afanye wepesi tuzifikie Jamii Zetu na kuzisaidia. Nia tunayo,Ari Tunayo tunahitaji support kutoka kwa Jamii yetu. Watu wetu Wakigoma bado wanahitaji kushikwa mkono na kutatuliwa shida zao. *#Jukumu letu*

๐Ÿ‘ 1
Video
Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
2/18/2025, 4:35:15 PM

*HII NI KWA MATUMIZI YA MTU YEYOTE ANAETOKA KIGOMA* Kumbuka anuani hii unaweza kuitumia na wewe katika shughuli zako za kiofisi na mambo yako mengine binafsi yaliyo halali, usisumbuke anuani ya kutumia, ikiwa tu hauna anuani mkoani Kigoma basi tumia anuani ya Jumuiya. Muhimu kutoa taarifa. JUMUIYA YA WATU WA KIGOMA S.L.P 734 KIGOMA, TANZANIA. Wilaya ya Kigoma, Kata ya Kigoma Mjini, Mtaa wa Shede, Barabara ya Bangwe na Stanley, Nyumba Na: 02 Barua pepe: [email protected] Namba ya simu +255744753493 .... Au ... KIGOMA PEOPLE'S COMMUNITY P.O.BOX 734 KIGOMA, TANZANIA Kigoma District, Kigoma Town Ward, Shede Street, Bangwe and Stanley Road, House No: 02 Email Address: [email protected] Phone Number +255744753493

Image
Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
2/20/2025, 6:20:15 AM

*WANAKIGOMA WALIOWAHII KUALIKWA /KUHOJIWA NA KUONESHA NJIA KUNAKO MAENDELEO YA MKOA WETU KUPITIA KADA MBALIMBALI KUPITIA WAO TUMEONA MABADILIKO MAKUBWA MKOANI KWETU* *TUNAOMBA KUWATAMBUA* *1-Hussein Kalyango:* Diwani kata ya Kigoma Manispaa ya Kigoma Ujiji 2015-2020. *2-Mr Kagoma:* Kiongozi wa Tembo FC Kibondo Kigoma. *3-Husna Sungura:* Kiongozi wa soka la Wanawake mkoani Kigoma *4-Ally Itembe* : Kiongozi wa soka mkoa wa Kigoma (General Coordinator wa TFF Kigoma) *5-Lulu Cement:* Kiongozi wa kurasa za Mashujaa FC *6-Chief LutaLosa Yemba:* Mgombea Urais Jamhuru ya Muungano wa Tanzania 2015 ADC *7-Dk Zimbwe Kauke* pharmacist (Dodoma Hospital) *8-Mh Hamisi Iddi mmasa* M/kiti Kijiji Cha Sunuka willaya ya UVINZA *Ccm*. *9-Mh Omari Gindi* mwekiti wa Chadema Wilaya kigoma mjini. *10-mwalim Banka the don* muonesha fursa Katavi. *11-Kolo Hamza malilo ll* Sultan wa wamanyema *12-Mbuya Ayoub kilima*. Makamu m/kiti chama Cha mpira wamiguu kigoma. *13-Hasan Hamis msimbwa* mfanyabiashara/Muonesha fursa na mshirika wachama Cha wafanyabiasha wamipakani.*Cross Border Traders Association CBTA* *14-Rashid Bakari Tanganyika* Meneja wa Taasisi ya *matwi Sports Academy* *15-Paul Wabike* Fursa za kibiashara Nchi za Ulaya. *16-Dr Mikota Karenga* (Masters Degree) Ufadhili wa Masomo Nchini Uturuki *17-Ernest Boniface Makulilo EBM*. Udhamini wa Elimu ya Juu Ughaibuni. *18-Jumbe Issa Jumbe* katibu wachama Cha mpira wamiguu Wilaya ya Kasulu. *19-Said Msonga* Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Ukanda wa Ulaya,Africa,Ulaya. *20-Mwalim Abuu Mvano* Afisa Uhamiaji mstaafu_kigoma. *21-Mh Shaabani Mambo* Mwanachama na Kiongozi wa ACT wazalendo_kigoma. --------- *Tunawashukuru sana na tuendelee Kushirikiana kwa Ajili ya maendeleo ya mkoa wetu Wakigoma* Wanakigoma mnakaribishwa ktk Mijadala mbalimbali ili kupanua fikra kwa Ajili ya maendeleo mkoani kwetu kigoma.

Image
Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
2/20/2025, 8:43:51 AM

*KIMBA ZIWANI -KIJIJI MWAKIZEGA-UVINZA* *Historia kwa ufupi wanaoisikia mwakizega* *Mapokeo* *Mtware Hadija wakizega* kutoka kabila la WATONGWE *TONGWE EMPIRE* ndio mtawala wa Eneo hili la Mwakizega.. Huyu Ndio aliwapokea Jamii ya Waarabu Ambao aliwapeleka mpaka Ilagala kwenda kulima mbaazi na kuvuna Sufi Mashambani kwa Ajili ya kutengeneza magodoro, Kati yahao Waarabu ni Mzee Ahmad Suod na Khalfan Soud ambaao walikua ni mkubwa na mdogo, Kutoa ktk Koo Hiyo ya watongwe Wazee Maarufu ktk Eneo hili ni Mzee *Katanga Mrisho Katanga* na *Athuman Mrisho Katanga (Nguvu ya mamba)* wote Hawa marehemu na HUYO mtawala alikua Dada yao. Kizega chini ya wajukuu *Mtware Bora wakizega na Bakari wakizega TONGWE EMPIRE* *#Utalii wandani* *#Mwakizega yetu* *#Uvinza yetu* *#kigoma yetu*

๐Ÿ‘ 1
Image
Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
2/22/2025, 7:22:06 AM

*UMOJA WA VIJANA WAKIGOMA KARIAKOO MWAKA 1980 RAHA STREET* *#Upendo* *#Nidhamu* *Kuheshimiana* *#Hii ndio kigoma*

Image
Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
2/22/2025, 7:29:04 AM

*BAADHI YA SAMAKI NA MAJINA YAO Ziwa Tanganyika* Mgebuka/Mkeke Nonzi Sangara Ndubu Manje Singa Malala Ndomondomo Kuhe Shanana Vijhole Kingongo Ntanga Nyika Msiha Mbanga Ngege Mbirigi Mbaraga Kakamsi Kavungwe Visarallah Kungura Nungi Mange Ndafa Somba Kikwera Kimizi Rumbu Mgara Mshekele Mrombo Vindulwa -Mzungu wachini -Kikarakacha -Kihongo -Mlangala *#Utalii wa ndani* *#Ziwa Tanyanyika* *#Ziwa lapili kwakina Duniani* *#kigoma Tanzania*

Image
Link copied to clipboard!