
IslamicForum
February 7, 2025 at 02:55 PM
USHINDI WA GHAZA.
Ni wiki kadhaa baada ya kutangazwa kusitishwa kwa mapigano baina ya jeshi la Makafiri lililojikusanya katika ardhi ya Waislam waliloliita Israeli wakiongozwa na America dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa ghaza. Ikiwa ni baada ya mwaka mmoja na miezi mitano. Ushindi hii tunaungalia katika maeneo haya yafuatayo.
1. Kijeshi katika uwanja wa vita.
2. Kiuchumi.
3. Kisiasi.
4. Kiitikadi.
5. Hatma ya kusitisha vita.
6. Mpango wa Trump kuhusu.
Kabla ya kuelezea hayo maeneo hayo tunapaswa kuangalia sababu za mujahidina wa ghaza kuingia katika vita hii. Mapambano hayo yamekuja Baada ya mujahidina wa ghaza kuingia katika ardhi iliyokoloniwa kwa mabavu na kuitwa Israeli kwa malengo haya yafuatayo.
A. Kuwatangalia mazayuni katika mpango wao, suala la ghaza kuvamiwa na kuvunjwa vunjwa na watu wake kuhamishwa lilikuwa jikoni linapikwa
Baada ya taarifa za kiintelijensia za kuaminika kwa mujahidina juu ya huo mpango. Njia sahihi kabisa iliyoonekana na kuwakabili hao majambazi kabla ya wao kuwaanza. Naam haya Sio mageni katika Uislamu hata sababu ya Mtume (s.a.w) kwenda Taabuk ni Baada ya kupata taarifa ya jeshi la kirumi kubwa linalojiandaa kuja kuivamia Madinah.
B. Kuwateka wanajeshi wa kiyahudi na kubadidilishana nao na waislamu walijazwa kwenye magereza ya Israeli Huku wakipata kila aina ya mateso.
C. Kuamsha kadhia ya Msikiti wa Aqswa na kujibu mabaya yenye kuendelea kufanywa katika Msikiti huo sambamba na wenye kwenda kuswali.
D. Kueneza hali ya uoga ndani ya Israeli ili wafahamu kuwa ardhi hii sio yao na wakati wowote wenye ardhi wataichukua.
E. Kuitikisa hali ya kisiasa ya Israeli na kuleta mpasuko katika serikali hiyo ya kigaidi.
F. Kugeuza mtazamo wa ulimwengu juu ya kadhia ya Ghaza na Palestina kwa ujumla.
G. Kuvuruga mipango ya utambuzi wa Serikali ya Israeli uliokuwa unafanywa na watawala vibaraka war nchi za Waislamu. (Normalization, التبيع)
Na baada ya hapo Israeli kwa ushirikiano na mataifa ya kimagharibi ikaingia ghaza ikiwa na kwa lengo la kukamilisha malengo haya yafuatayo.
A. Kukifuta kizazi cha watu wa ghaza.
B. Kuikoloni ghaza.
C. Kuwahamisha watu wa ghaza.
D. Kumaliza uongozi wa Hamas katika ardhi ya Ghaza.
E. Kurejesha mateka kwa nguvu za jeshi.
F. Kufunga mpaka wa Rafah.
H. Kuwahamisha viongozi wa Hamas.
I. Kukalia kimabavu eneo la Tishaim na Filadefia.
J. Kujenga makaazi ya walowezi ghaza.
K. Kutekeleza hatua ya majenerali.
L. Hatua ya siku inayofuata baada ya kuifuta Hamas.
M. Kuendelea kuizingira ghaza na kuidhoofisha kwa njaa.
Kwa sura ya wazi mpaka vita vinasitishwa ushindi ni kwa mujahidina wa ghaza kwa kufikia malengo yao yote, na jeshi la muungano wa makafiri kutofikia lengo hata moja.
KIJESHI KATIKA UWANJA WA VITA.
kutokana na Malengo ya mujahidina hao waliingia vitani wakijua uzito na ukubwa wa vita hivyo, Sio kwamba waliingia wakijua kuwa wa jeshi kubwa zaidi ya makafiri, wana silaha nzuri zaidi yao, wana bajeti nzuri zaidi yao laa hasha waliingia kwakuwa wamedhulumiwa haki yao, unadhalilishwa Msikiti mtukufu na wakijua kuwa nusra yako Allah ikiwa upande wao.
Mujahidina walijizatiti katika idara zote za kivita na katika intelinjensia, kuhifadhi mateka, matumizi sahihi ya silaha zao Huku wakijua kuwa hawana msaada wowote kutokana kwa binadamu, media kuku kuchagua staili ya kupiga na kuondoka (gorilla war). Mujahidina wa ghaza kwa ujumla wao hawavuki elfu 50.
Wamekabiliana na jeshi lenye kila aina za silala za kisasa lenye kupata msaada wa kila aina kutoka Katika nchi za kimagharibi kuanzia fedha, silaha na wanajeshi. Askari mamluki kutoka Katika mataifa ya kimagharibi, Afrika, Asia yaliyopeleka askari wake ghaza yanavuka 22 Huku askari hao mamluki ni zaidi ya elfu 50.
Viongozi wa Mujahidina wa ghaza walijua gharama ya vita hivyo kwa hivyo waliwaanda waislam wa ghaza juu ya yajayo wao wakiwa mstari wa mbele katika mapambano hayo naam dunia imeshudia viongozi hao wakiwa Safu ya mbele yake mapambano na wote wamekufa Mashahidi Allah awarehemu wanaume hao Wakina Yahya Sinwaar kiongozi wa Hamas, Muhammad Dheif mkuu wa jeshi la mujahidina Ismaili Haniya kuu wa ofisi ya kisiasa na wengineo.
Katika mapambano hayo mujahidina wa ghaza zaidi ya elfu 8 wamakufa Mashahidi huku wakiwapeleka Jahannam wanajeshi wa jeshi la muungano zaidi ya elfu 30 na majeruhi zaidi ya elfu 50, waliopata wazimu zaidi ya elfu 3.....
Inaendelea.......
By Sheikh Khatibu Imran Abuu khaliil
😢
1