IslamicForum WhatsApp Channel

IslamicForum

157 subscribers

About IslamicForum

IslamicForum: for Islam, News and Interact.

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

IslamicForum
IslamicForum
5/15/2025, 4:44:13 PM

Bendera walizokuwa wakibeba za Uislamu zimetupwa na kupandishwa bendera ya Ukoloni na Kilemba kimetupwa mwendo wa suti na tai, sasa ni mwendo wa kukumbatia Maadui na kuwa kibaraka wao mtiifu tena kwa kuinamisha kichwa chini!. Ni suala la muda tu utakuwa dhalili kama si hapahapa duniani basi kesho Akhera.

Post image
Image
IslamicForum
IslamicForum
5/14/2025, 4:14:32 PM

HAMAS JANA WALIMWACHILIA MWANAJESHI WA ISRAEL, EDAN ALEXANDRER

Post image
Image
IslamicForum
IslamicForum
5/16/2025, 9:05:04 AM

Na historia iandike: Kwamba Trump aliingia katika kisiwa cha Waarabu "Jaziratul Arab", akakikuta hakina wanaume… kimejaa watumishi… kimejaa dhahabu… lakini kimefilisika heshima na utukufu! Trump hakutudhalilisha kwa silaha, bali kwa tabasamu. Wala hakutushinda kwa jeshi, bali kwa simu ya maongezi! Basi ni udhalili wa aina gani huu? Na ni Uislamu gani uliobakia ikiwa hatuoni katika tukio hili usaliti wa zama? Enyi watu… Hakika adui wa Mwenyezi Mungu, Trump, hakuingia katika ardhi ya Haramain kama mwizi kutoka baharini, wala kama mvamizi kwa ndege, bali aliingia kwa kupitia milango ya miji ya kifalme, katika msafara wa fahari, akipokewa kama "Faatihina" mashujaa washindi! Akapokelewa kwa heshima kuu, akapewa hazina ili achukue apendacho! Viongozi walimlaki kwa mfululizo, shingo zikalazwa mbele yake, watu wa mafuta na uamuzi wakamtolea heshima kama kwamba wahyi umeshushwa juu yake kutoka Jabal Radwa! Na kule Qatar… Washauri wa Amir na wakubwa wa dola wakamsogelea, si kama kiongozi wa taifa, bali kama...👇

Post image
Image
IslamicForum
IslamicForum
5/15/2025, 5:22:18 PM

𝗜𝗧𝗔𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔👇 √ Pakistan lilikuwa ni Taifa lenye nguvu za nyuklia, lakini halikuweza kutoa msaada kwa Palestina hata kwa uchache wa risasi tu. √ Misri ilikuwa na mto Nile, lakini Wapalestina wa Gaza hususan watoto wadogo walikufa kwa Kiu kikali. √ Saudi Arabia na UAE walikuwa na bahari za mafuta, lakini hospitali za Gaza na gari za wagonjwa (Ambulances) hazikuwa na mafuta ya kuendeshea. √ Itakuja kukumbukwa kuwa, Mataifa ya Kiislamu yalikuwa na zaidi ya Wanajeshi milioni 5, mizinga mizito, makombora ya masafa marefu, na ndege za kivita, lakini hakuna hata kimojawapo kilichoweza kufika Gaza na kutoa msaada. Hata kama Palestina leo itakuwa huru na Taifa la Israel kufutika katika ramani, Kizazi kijacho hakitashangazwa na mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Israel kwa Wapalestina, bali kitashangazwa na ukimya wa kutochukua hatua wa Mataifa ya Kiislamu ilhali uwezo huo walikuwa wanao. ___ By: Rmunga Credit: Moaz Majeed

Post image
Image
IslamicForum
IslamicForum
5/14/2025, 12:50:41 PM

Rais Trump wa Marekani atangaza kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Syria.

Post image
Image
IslamicForum
IslamicForum
5/16/2025, 4:52:51 AM

Msemaji wa Hamas, Abu Ubaida: Trump amekwenda Saudi Arabia, kutafuta kuungwa mkono na ulimwengu wa Kiarabu. Lakini sisi tunamtegemea Mwenyezi Mungu pekee ambaye amewahi kuwaangamiza Firauni wengi kabla yake.

Post image
❤️ 🙏 3
Image
IslamicForum
IslamicForum
5/16/2025, 10:41:29 AM

Zaidi ya Wapalestina 100 waliuawa katika mashambulizi kadhaa yaliyofanywa na jeshi la Israel kaskazini mwa Gaza alfajiri ya leo. Vyanzo vya matibabu viliiambia Shirika la Anadolu kwamba jeshi la Israeli lilifanya "mauaji ya kutisha" yakilenga raia. Waliripoti majeruhi kadhaa wakati jeshi la Israeli lilipolenga gari la wagonjwa katika mji wa Jabalia kaskazini mwa Gaza, shambulio la hivi punde zaidi katika mfululizo wa mashambulizi dhidi ya madaktari na vituo vya afya. Mwandishi wa Anadolu pia aliripoti kuwa jeshi la Israel lililenga zaidi ya nyumba 11 zinazokaliwa na watu kaskazini mwa Gaza. Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya huko Gaza alithibitisha kwamba Ukanda huo "unashuhudia mauaji ya kikabila ambayo yamesababisha mauaji ya watu 250 ndani ya masaa 36 tu," akiashiria kulengwa kwa utaratibu kwa hospitali na uvamizi. Aliongeza kuwa uvamizi huo unatumia silaha za kisasa zilizopigwa marufuku kimataifa kulenga vituo vya kiraia, akitaka uchunguzi wa kimataifa kuhusu aina za silaha hizo zilizopigwa...👇

Post image
Image
IslamicForum
IslamicForum
5/16/2025, 9:05:06 AM

Na historia iandike: Kwamba Trump aliingia katika kisiwa cha Waarabu "Jaziratul Arab", akakikuta hakina wanaume… kimejaa watumishi… kimejaa dhahabu… lakini kimefilisika heshima na utukufu! Trump hakutudhalilisha kwa silaha, bali kwa tabasamu. Wala hakutushinda kwa jeshi, bali kwa simu ya maongezi! Basi ni udhalili wa aina gani huu? Na ni Uislamu gani uliobakia ikiwa hatuoni katika tukio hili usaliti wa zama? Enyi watu… Hakika adui wa Mwenyezi Mungu, Trump, hakuingia katika ardhi ya Haramain kama mwizi kutoka baharini, wala kama mvamizi kwa ndege, bali aliingia kwa kupitia milango ya miji ya kifalme, katika msafara wa fahari, akipokewa kama "Faatihina" mashujaa washindi! Akapokelewa kwa heshima kuu, akapewa hazina ili achukue apendacho! Viongozi walimlaki kwa mfululizo, shingo zikalazwa mbele yake, watu wa mafuta na uamuzi wakamtolea heshima kama kwamba wahyi umeshushwa juu yake kutoka Jabal Radwa! Na kule Qatar… Washauri wa Amir na wakubwa wa dola wakamsogelea, si kama kiongozi wa taifa, bali kama “mkombozi” anayepaswa kutiiwa. Na kule Emirates… Akapokewa kwa namna ambayo hata wafalme wa zamani hawakuwahi, hadi wanawake wakamchezea densi kama kwamba wao ni warembo wa hadithi za “Alfu Lailah wa Lailah”, lakini kwa mdundo wa tamaduni za Kimarekani, si mashairi ya Kiarabu! Ngoma yao haikuonyesha ukarimu, bali ilidhihirisha unyenyekevu wa aibu, na Hadhara iliyoporomoka ikikanyagwa na mnyanyasaji huku ikimchekea. Usiulize kuhusu jizya (kodi ya aibu)! Hazina zilifunguliwa kwake bila masharti, akapewa kutoka kwa mali ya Waislamu kile ambacho hata mkoloni asingethubutu kuomba kwa jeshi lake. Ni “jizya ya ridhaa”... haichukuliwi kwa hofu ya upanga, bali kwa tamaa ya kukubalika! Na uvamizi haukusimama kwa mali tu, bali ukaenda hadi kwenye dini na heshima… Trump akaketi na mtumishi mpya wa Damascus, mtu aliyewahi kuijaza dunia kwa hotuba kuhusu jihad na ukombozi wa al-Aqsa na waja, lakini sasa anamkalia mbele adui wa Allah kama afisa wa uhusiano wa umma, akisikiliza, anatabasamu, kisha anakubali kuingia kwenye njia ya kusaliti Quds kwa jina la “Tatbii'” Hali ya kawaida na Mayahudi. Enyi watu… Kilichotokea si ziara ya kawaida. Ni tangazo la kifo cha kihadhara mbele ya kamera! Kama Ummah unampokea muuaji wake kwa kumbatio, linamwekea zulia jekundu, linamweka kwenye viti vya heshima – basi ujue kwamba maadili yamesambaratika, na historia inaandikwa kwa herufi za aibu na fedheha! Mapokezi haya siyo siasa – ni aibu. Siyo diplomasia – ni ishara ya kuanguka. Trump aliingia ardhi ya Waarabu, akawakuta watawala wasio na haiba, majeshi bila aqeeda, wanazuoni wasio na sauti, na wasomi wapiga makofi, huku watu wakiwa kimya kwa unyonge… isipokuwa wale waliobakia na pumzi ya heshima! Enyi watu wa nguvu... Enyi mliohifadhi ndani ya nyoyo zenu ukumbusho wa Uislamu na urithi wa utukufu… Je, si wakati wa kuinua vichwa kutoka katika aibu hii? Je, si wakati wa kuvunja minyororo ya unyenyekevu huu? Je, si wakati wa kutakasa tena ardhi ya Jazira, si kwa kuondoa masanamu ya mawe, bali masanamu ya kibinadamu yanayoitawala leo? (Enyi mlioamini! Atakayeiacha dini miongoni mwenu, basi Mwenyezi Mungu atakuja na watu wengine, anawapenda na wanampenda, wanyenyekevu kwa Waislamu, wenye nguvu dhidi ya makafiri, wanapigana jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya mwenye kulaumu. Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua. (Al-Ma’idah: 54) – Mundhir Abdullah

IslamicForum
IslamicForum
5/14/2025, 2:07:02 PM

Matakwa ya Donald Trump kutoka kwa Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa kulingana na Ikulu ya White House: 1. Ingia kwenye Makubaliano ya Abrahamna Israeli 2. Waambie "magaidi" wote wa kigeni kuondoka Syria 3. Wafukuze “magaidi” wa Kipalestina 4. Saidia Marekani kuzuia kutokea tena kwa ISIS 5. Chukua jukumu la vituo vya wafungwa vya ISIS Kaskazini Mashariki mwa Syria.

Post image
Image
IslamicForum
IslamicForum
5/14/2025, 6:14:31 AM

India - Msichana wa Kiislamu Alibakwa na Kuuawa Msichana wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 10 alibakwa na kuuawa na jirani yake huko Saharanpur, Uttar Pradesh. Alikuwa akicheza nje ya nyumba yake Ijumaa jioni wakati mshtakiwa alipomteka nyara na kumbaka. Kwa kuhofia kwamba angekamatwa, mshtakiwa alimnyonga hadi kufa na kuuficha mwili huo msituni umbali wa mita 200 tu kutoka nyumbani kwake. Polisi walimkamata jirani yake; Vedprakash Dhiman mwenye umri wa miaka 50.

Post image
Image
Link copied to clipboard!