IslamicForum
IslamicForum
February 8, 2025 at 03:40 PM
UTEGEMEZI WA DAWA NA VIFAA TIBA NI DHIHIRISHO LA UDHAIFU WA MATAIFA YA AFRIKA MBELE YA MABEPARI Na, H.Nditi Juzi katika hotuba yake Rais wa Amerika Donald Trump alitoa tamko la kusitisha ufadhiri wa dawa za ARV kwa mataifa masikini, na badala yake kuwataka kulipia dawa hizo. Kauli hii ya Trump imeambatana na msululu wa matamko mbalimbali kama vile kuiondoa Amerika katika shirika la Afya duniani(WHO), katazo la jinsia nyingi, na kurejesha wahamiaji haramu. Kwa muda mrefu toka miaka ya 1950s shirika la USAID linaendesha huduma na misaada ya afya na tiba kwa mataifa machanga. Shirika hili limekuwa likiidhinisha mikopo ya dawa pamoja na kufadhiri dawa za ARV kwa wagonjwa wa UKIMWI duniani. Kwa mujibu John Pertikns ambae ni mwandishi wa kitabu cha Secret of America Empire, ameandika kuwa mashirika kama ya USAID, taasisi za filamu na yale ya ujenzi huwa yanatumika kama vyombo vya kimkakati ili kutimiza lengo la Amerika kunyonya rasilimali za nchi masikini. Taasisi hizi huwaingiza mataifa duni katika...👇

Comments