IslamicForum
IslamicForum
February 8, 2025 at 03:40 PM
UTEGEMEZI WA DAWA NA VIFAA TIBA NI DHIHIRISHO LA UDHAIFU WA MATAIFA YA AFRIKA MBELE YA MABEPARI Na, H.Nditi Juzi katika hotuba yake Rais wa Amerika Donald Trump alitoa tamko la kusitisha ufadhiri wa dawa za ARV kwa mataifa masikini, na badala yake kuwataka kulipia dawa hizo. Kauli hii ya Trump imeambatana na msululu wa matamko mbalimbali kama vile kuiondoa Amerika katika shirika la Afya duniani(WHO), katazo la jinsia nyingi, na kurejesha wahamiaji haramu. Kwa muda mrefu toka miaka ya 1950s shirika la USAID linaendesha huduma na misaada ya afya na tiba kwa mataifa machanga. Shirika hili limekuwa likiidhinisha mikopo ya dawa pamoja na kufadhiri dawa za ARV kwa wagonjwa wa UKIMWI duniani. Kwa mujibu John Pertikns ambae ni mwandishi wa kitabu cha Secret of America Empire, ameandika kuwa mashirika kama ya USAID, taasisi za filamu na yale ya ujenzi huwa yanatumika kama vyombo vya kimkakati ili kutimiza lengo la Amerika kunyonya rasilimali za nchi masikini. Taasisi hizi huwaingiza mataifa duni katika mitego ya misaada na mikopo mikubwa, ambayo hawataweza kulipa ili waweze kuweka rehani rasilimali zao kama njia ya kurejesha fedha. Kitendo cha Amerika kuacha kufadhiri dawa hizi, ni dhihirisho kuwa lengo la Amerika kuchota mali za nchi changa limefanikiwa. Amerika kupitia taasisi zake imeweza kuchota madini na mafuta ya kutosha kutoka Asia, Uwarabuni na Afrika. Hivyo kitendo cha kuzitaka nchi hizi zinunue madawa ni wazi analengo za kuzinyonya zaidi hasa baada ya kuziona zinajikurubisha kwa China na Urusi. Mbali na unyanyasaji huu, tamko hili la Trump limeweza kufichua uduni wa mataifa ya Afrika hasa Kusini mwa jangwa la sahara. Mataifa haya yamekuwa yakipewa sifa bandia na taasisi za Amerika kama Benki ya Dunia na IMF kuwa zimekuwa kiuchumi ilhali mambo tofauti na uhalisia. Nchi za Kibepari zimetawala kila sekta na kutumia nguvu yao kunyonyo mataifa haya. Wameminya nchi changa kutumia formula zao za madawa ili waendeleze utegemezi wa dawa kutoka kwao. Hata hivyo, japo nchi za kibepari zinaweka vizuizi kwa nchi changa kutumia formula zao za madawa, ila wanaouwezo wa kuwekeza akili na maarifa kutafuta tiba za magonjwa na chanjo mbalimbali. Lakini hatuna jitihada hizo kwa serikali na badala yake wanaendekeza utegemezi. Tamko hili la Trump kwa upande mwengine linadhihirisha uhusiano wa kinyonyaji baina ya Afrika na Mabepari. Hakuna ushirika wa kweli kutoka kwa nchi za Kimagharibi, China na Urusi. Watazitazama nchi za Afrika kama sehemu ya kuchota mali na kuondoka. Ni muda muafaka sasa kwa nchi za Afrika kutafuta namna ya kujikomboa katika mfumo wa kidemokrasia na ubepari na badala yake kuchukua mfumo mwengine hasa Uislamu ili waweze kupiga hatua.

Comments