IslamicForum
February 12, 2025 at 08:33 AM
#kwanini_saud_imebadili_msimamo WAKE JUU YA #mwezi MWANDAMO?
Awali tulimesema mara kadhaa kwamba suala hili la ikhtilafu juu ya mwezi mwandamo kwa miaka ya hivi karibuni lina simamiwa na wanasiasa kuugawa umma wa kiislamu
Na wala halipo tena kifiq’hi kama hapo awali zama za kina Imamu Shafy na wenzake walio ikhtilafiana juu ya mwezi mwandamo
Mizozo ya leo juu ya mwezi ni maagizo tu ya watawala pasina kujali wala kuzingatia ikhtilafu za fiq’h
Wakoloni wamewapa maagizo vibaraka wao kwa kuzipangia nchi juu ya kufunga na kufungua kuhakikisha waislamu hawaungani juu ya nembo hii kubwa ya umoja wa umma wa kiislamu
Basi mwezi utatangazwa nchi fulani hata kama haukuandama na utakataliwa nchi ya pili hata kama ume andama
Na hili lipo wazi kiasi kwamba halihitaji hata kutoa ushahidi
Utakuta nchi hii inafunga lakini nchi jiran haifungi na hata raia walio mipakani mwa nchi iliyo funga hawa ambiwi basi wao wafunge kwani wapo jirani na nchi ambayo mwezi umeandama kwa kuzingatia hoja ya masafa wanayo ipigia kelele
Mfano mwezi uonekane Kenya basi mtu wa Lungalunga ya Kenya atafunga pamoja na mtu wa Migori ya Kenya umbali zaidi ya kilo mita 1000
Lakini mtu wa Horohoro ya Tz hafungi pamoja na mtu wa Lungalunga ya Kenya licha kwamba ni umbali wa mita 3 tu
Bali mtu wa Horohoro TZ atasubiri kufunga pamoja na mtu wa Mbeya TZ umbali zaidi ya kilo mita 1,300 je hii ni ikhtilafu ya ki-fiq,h au ni maagizo ya ki-siasa?
Ni kweli sheria ya Allah imebadilika baada ya wakoloni kuchora hii mipaka?
Leo Imam Shafy angekuwa anaishi Horohoro ya TZ na mwezi ukaonekana Lungalunga Kenya asinge funga kwa sababu yeye sio Mkenya na angesubiri mwezi wa Chunya Mbeya au Manyovu Kigoma?
Hivyo mwislamu yeyote anaye funga na kufungua kwa kuathiriwa na mipaka hii ya wakoloni ajue anayo kesi ya kujibu siku ya qiyama wala hana udhuru kwamba masheikh wangu walinambia nifunge au nisifunge kwa sababu ya mambo ya nchi mipaka na uzalendo
Makundi yote yaliyo kuwa yana zozona na kutukanana juu ya mwezi mwandamo yalikuwa yanatetea uzalendo na mipaka zaidi kuliko kutetea hukmu ya kisheira ya uislamu
Wanao tokwa na jasho kutetea mwezi wa kitaifa ilikuwa ni uzalendo na walio kuwa wanatokwa na jasho kutetea mwezi wa Saud kwa kutumia kichaka cha mwezi wa kimataifa ilikuwa ni kuchunga posho kutoka Saud au mapenzi ya masheikh wake wa Kisaud
Na ndio sababu mwezi ulipo andama nje ya Saud na Saud ikaukataa basi na wao hawakufunga wala kufungua
Kama tulivyo shuhudia miaka ya hivi karibuni
Kwanini leo masheikh wa fikra za Saud wamebadili misimamo au kupunguza ukali juu ya mwezi mwandamo?
Ni kijana MBS amebadili msimamo ya Saud kwa % kubwa na misimamo mingi iliyo kuwa imeshikiliwa na Saud kwa jina la uislamu ilikuwa ni maslahi ya kisiasa wala si kidini kama alivyo tamka wazi MBS mwenyewe bali alikwenda mbali zaid kwa kusema hata baadhi ya misimamo iliyo vishwa guo la dini yalikuwa ni maagizo ya Amerka
Hivyo tutarajie kuachwa na kutupiliwa mbali bali hata kupigwa marufuku kabisa misimamo kadhaa wakadhaa
Na huenda pia Saud imelalamikiwa na watawala wa nchi zingine kwa madai ya uongo ya kuvuruga mshikamano wa mataifa yao kwa kuwepo masheikh katika nchi zao wanao pokea maagizo ya mwezi kutoka Saud badala ya kutoka nchi wanazo ishi
Au ni Saud yenyewe inataka mahusiano mema na nchi zingine kwani ndoto ya 2030 aliyo oteshwa MBS na shetani ndoto hiyo inahitaji uhusiano mkubwa sana na nchi zote duniani ili walevi wengi na malaya wasiogope kwenda Saudia
Basi leo tutarajie mizozo hii ya mwezi kwisha au kupungua kutoka kwa wafuasi wa Saud dhidi ya masheikh wa kiserikali za kitaifa
Na si mwezi tu, bali watakubali muda si mrefu mpaka maulidi, khitma, dufu, na kuzuru makaburi.
ni suala la muda tu
Ima wataunga mkono wazi wazi au wataacha kabisa kuzungumza mambo hayo kwa madai kwamba ni uzushi
Kwani agenda ya MBS sio makaburi na maulidi bali ni utiifu tu kwa tawala hivyo vita yao leo masheikh wa Kisaud ni ukhawaarij na u-hizbiyat na si zaidi
Je msimamo sahihi ni upi?
Huku tukiheshimu waislamu wengine wenye msimamo tofauti na wetu
Lakini msimamo sahihi ni msimamo wa mwezi mwandamo mmoja tu
Na tofauti itabakia ni kwenye masaa
Huu ndio msimamo sahihi
Na msimamo huu sio ule wa Ki-saud kudai ni mwezi wa kimataifa lakini mataifa yenyewe ni Saudia peke yake tu!
Na lau mwezi utaandama nchini Zimbabwe kwa mfano basi wao hawato funga swaumu au kufungua swaumu.
Huo sio msimamo wa kidini bali ni msimamo wa kidinari au mapenzi ya kibubusa kwa masheikh wa Ki- saud ambao wote ni watumishi wa wafalme kwa maslahi ya wafalme
Kwanini hoja hii ya mwezi wa kimtaifa inakuwa na nguvu zaidi?
1 leo imebainika wanao shikilia ikhtilafu za masafa ni mapenzi au utumishi wa nchi zao na sio hukmu ya kisheria
2 wameshindwa kufafanua mwisho ni masafa kiasi gani kisheria je ni kilo mita 3 au 67 au 200? Hawawezi na hawato weza kujibu swali hili hivyo ni kushikilia msimamo usio kuwa na ufafanuzi
3 hukmu ya kisheia panapo tokea mzozo wa mambo yenye ikhtilafu na pande mbili wote wakawa na hoja lakini hoja zao wote ni hoja za dhana (ijtihaadi) basi umoja wa uislamu hutatangulizwa kwani hakuna ikhtilaf juu ya uwajibu wa umoja wa waislamu bali ni dharura katika dini waislamu kulinda umoja wao
Na mwezi mwandamo mmoja dunia nzima ni ishara ya umoja wa uislamu duniani bila shaka wala ikhtilafu yoyote
Na kushikilia miezi ya kila taifa na mwezi mwandamo wake ni hoja inayo vunja umoja waislamu duniani
Hivyo hoja ya mwezi wa kitaifa hata ingekuwa na mashiko basi mashiko yake ni ya dhana (ijitahd) huangushwa na hukmu ya umoja ambayo ni muhkamu (qat,iyy)
Ama hoja za tofauti ya kuingia usiku na mchana itabakia kama ilivyo ,kwamba yatatofautiana masaa
Kama tuonavyo wazi hata kwenye siku kuu zao za kimataifa,
mfano mwamka mpya,
hakuna wanao sherehekea siku yapili bali huwa ni tofauti tu ya masaa
Nchi gani mwaka mpya husherehekea tarehe 2 January?
Allah atufikishe salama Ramadhani na atujaalie kupata kheri zake
Abuu Fat,h Sheikh Ramadhani Moshi Othman. 03—02—2025