IslamicForum
February 12, 2025 at 12:06 PM
TUNAISHI KATIKA ZAMA MBOVU NASAHA ZA KUIFUATA QUR'AN KUTOKA KWA KAFIRI.
Tunaishi katika zama mbovu sana, leo Waislamu kwa fikra duni wanaitumia Qur'an kuimarisha ukafiri (uzalendo na demokrasia). Kwasasa Qur'an inatumika kama sehemu ya kampeni za nidhamu ya kikafiri ya kibepari na demokrasia, hali kadhalika inatumika kuotesha mizizi ya fikra ya kiuzalendo ambayo kiongozi fikra ya kikafiri.
Bado haitoshi leo makafiri ndio wanakuwa wageni waalikwa nao wanakuja kutoa nasaha kwa Waislam kuifuata Qur'an. Nukuu.
Dk. Biteko amesema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Mashindano Makubwa zaidi ya Qur’aan Tukufu Ulimwenguni 2025.
“Nawaomba msivunjike moyo akitokea mwenye tafsiri tofauti nyie msivunjike moyo wala kukatishwa tamaa bali mfanye mashindano haya yawe kinara na kuutangaza uislamu katika ulimwengu,” amesema Dkt. Biteko.
Pia amewahimiza kumuomba Mungu ili Qur’aan iwanyanyue na isiwabwage katika shughuli mbalimbali wanazofanya kama kaulimbiu ya mwaka huu inavyosema “ Qur’aan Ikunyanyue,...👇