
IslamicForum
February 28, 2025 at 06:50 PM
MAKHATIBU WA IJUMAA LEO WAELEZENI WAISLAMU MAMBO HAYA
Leo inshaAllah ndio Ijumaa ya mwisho wa mwezi wa Shaaban, ambapo siku yoyote kuanzia kesho inshaAllah tutaingia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Katika hali kama hiyo tunawasihi na kuwaomba kwa dhati kabisa makhatibu kesho katika mimbar zao wawaeleze Waislamu yafuatayo:
1. Swaumu ya Ramadhani imeletwa kwa lengo la kumcha Allah Taala. Na asili uchamungu ni jambo la muda wote. Maana yake ni kuwa Waislamu waubebe uchamungu ndio dira ya kila siku ya maisha yao.
2. Kwa sababu Swaumu inatuhimiza uchamungu, na kwa sababu uchamungu wa kweli hauwezi kufikiwa ila pawe na utawala wenye mamlaka kamili ya kuulinda. Ina maana kuwa Ramadhani inatuhamasisha tutawaliwe chini ya mfumo wa Kiislamu kwa kuwa ukamilifu wa taqwa hutegemea utawala wa Kiislamu (Khilafah) na si kinginecho.
3. Swaumu ni ibada ya Waislamu tu, na ndio maana amri yake ikaanza na mwito wa: ‘Enyi Mlioamini’. Hivyo, masuala ya kujumuika na wasiokuwa Waislamu katika mchakato wa ibada hii kama...👇