AJIRA FASTA FORUM
AJIRA FASTA FORUM
February 24, 2025 at 09:54 AM
Uongozi wa shule ya Awali na Msingi ya Eden Valley iliyoko Jijini Mwanza unatangaza nafasi za kazi ya Ualimu kwa walimu wenye sifa, uwezo na uzoefu wa kufundisha masomo yafuatayo: 1. Mathematics na Science kuanzia Darasa la III hadi Darasa la VII.Nafasi Moja. 2. Kifaransa kuanzia darasa la I hadi darasala IV SIFA ZA MWOMBAJI : 1. Awe amesomea taaluma ya Ualimu toka vyuo vinavyotambulika 2. Awe na uzoefu wa kufundisha masomo husika kwa angalau miaka miwili. Usaili utafanyika shuleni EDEN VALLEY mtaa wa Bulola A, Buswelu siku ya juma nne, tarehe 25Februari,2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi. Mwombaji afike na barua ya maombi, Wasifu wake (CV) pamoja na vyeti halisi vya kitaaluma. Mawasiliano: 0757905508/0672770252

Comments