
Kingstoretz
February 13, 2025 at 09:49 PM
Kimi AI 1.5 ni modeli mpya ya akili bandia (AI) iliyotengenezwa na kampuni ya Moonshot AI kutoka Beijing, China. Hii ni aina ya akili bandia inayoweza kuelewa na kuandika maandishi kwa ufasaha.
🔹 Inaweza kusoma na kuchambua maandishi marefu – inaweza kushughulikia hadi maneno milioni 2 kwa mara moja, jambo linaloifanya iwe bora kwa kuchambua nyaraka kubwa na kazi ngumu.
🔹 Ina uwezo wa kutafsiri picha, maandishi na hata kuandika programu – inatumia teknolojia ya hali ya juu kusoma taarifa za picha.
🔹 Ni bure – tofauti na AI nyingi ambazo zinahitaji malipo ya kila mwezi, Kimi AI 1.5 inapatikana bila gharama kupitia tovuti au app yake, bila hata kuhitaji akaunti.
🔹 Inapewa sapoti kubwa na wawekezaji wakubwa wa teknolojia nchini China – kampuni inayoitengeneza ina thamani ya dola bilioni 3.
🔹 Imepewa sifa nyingi kwa uwezo wake wa kushughulikia maandishi marefu na kupata taarifa mpya kwa haraka.
Kazi ambazo ChatGPT inahitaji mtu kulipia zaidi ya 50,000 mpaka 200,000; akili bandia hii inazifanya bure.
❤️
1