Mwanzo TV
February 25, 2025 at 07:46 AM
#uganda: *MWANASOKA WA NIGERIA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA KUTOKA KWA GHOROFA YA TATU, UGANDA*
Mwanasoka wa Nigeria, Abubakar Lawal, amefariki baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tatu ya jengo la ununuzi huko Kampala, Uganda.
Lawal, ambaye alikuwa mshambuliaji wa klabu ya Vipers SC, alikuwa akimtembelea rafiki yake wa Kitanzania katika moja ya vyumba vya makazi ndani ya jengo hilo wakati tukio hilo lilipotokea.
Polisi wa Uganda wameanzisha uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kukagua picha za CCTV na kufanya mahojiano ya kina. Klabu ya Vipers SC imetoa taarifa ya huzuni, ikieleza kuwa kifo cha Lawal ni pigo kubwa kwa klabu na jamii ya soka.