Mwanzo TV
February 25, 2025 at 12:34 PM
#tanzania: *CHADEMA YAFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA*
Mapema leo tarehe 25/02/2025, Mwenyekiti wa @ChademaTz Taifa @TunduALissu akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara @HecheJohn Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara Amani Golugwa na Mjumbe wa Kamati Kuu @godbless_lema Lema wamekukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Tine Tonnes katika makazi ya balozi Oysterbay, Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo Mwenyekiti Lissu pamoja na ujumbe wake wamekuwa na majadiliano na Balozi Tine kuhusu msimamo wa chama cha CHADEMA wa "No Reforms No Elections" na umuhimu wa Jumuiya za Kimataifa kushiriki, kuisaidia na kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo bora wa kiuchaguzi, iliyo ya wazi, ya haki na kuaminika katika kuendelea kujenga demokrasia nchini.
Balozi alimuhakikishia Lissu kuwa Norway itaendelea kuwa rafiki mwema wa Tanzania katika kudumisha demokrasia na maendeleo ya watu.