TaifaHouse
February 7, 2025 at 05:18 PM
*Nikafika kwa Da Zuu*
Basi bwana, nikasema leo nipite kwa wana niliosoma nao IFM miaka 13 iliyopita. Kwakuwa mimi nilikuwa Waziri Mkuu nikasema nianze na aliyekuwa Spika wa Bunge IFMSO 🥷.
Amefungua yard yake maeneo ya Kinondoni, nikaenda. Baada ya kupiga story mbili tatu, nikasema twende lunch na ninavyopenda kula sasa.
Akanipeleka hapo kwa Da Zuu, embwana wee, mmmh asikwambie mtu. Kwanza picha linaanza magari 4x4 yamepaki ya kutosha STM, STN, Benz, BMW, WildTrack n.k magari yote makubwa, na sisi kwenye kigari chetu cha yard bado kipo sokoni hao hatuko nyuma sana 🤣🤣🤣 of course ni gari nzuri nzuri.
Tumeshuka tu, nikadhani kuna msiba, watu wamejaa, ni eneo la uwanja wa nje ya nyumba karibu na barabara, juu kuna maturubai yamefungwa upande mwingine umeachia, pengine hakuna kabisa maturubai, chini hakuna kitu cha ziada zaidi ya udongo na mfereji wa maji, viti vya kukaa havitoshi baadhi ya watu wanakula wamesimama, yaani chakula kinagombaniwa na watu wenye heshma mjini. Chakula cha 👉👉👉👉 Next