TaifaHouse
TaifaHouse
February 7, 2025 at 05:21 PM
*Nikafika kwa Da Zuu* Ep02 Inaendelea.. Chakula cha bei rahisi ni noti ya Sh. Elfu 10 yenye sahihi ya Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, hiyo sinia hapo juu ni elfu 30. Basi bwana tukapanga foleni ya kuagiza kwenye kibanda ambacho na chenyewe kipo nje, juu hapajafunikwa, ni kama vile vibanda vya magenge ya kuuzia nyanya, na foleni yenyewe hakuna anaejua nani alitangulia, ni watu tumezunguka kibanda tumenyoosha pesa mbele 😂😂😂😂 yaani mwenye sauti kubwa ndo anasikilizwa. Baada ya dakika 10 tukapakuliwa chakula kwenye sinia kama hapo juu. Kazi ikaanza kutafuta meza na siti, tukabahatisha meza wamekaa watu 2, tukagongea na sisi tukaweka sinia yetu, tukaenda kunawa kwa ajili ya kula. Jirani ya Da Zuu ni Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata, na kulia kuna mgahawa mzuri sana wa kisasa tena unafahamika sana, lakini watu hawaendi kula pale, wanakuja kwa Da Zuu. Chakula cha Da Zuu kweli ni kitamu, nikamuuliza rafiki yangu, vipi hizi juice kila mtu anakunywa nataka niagize, akaniuliza unakunywa maji yetu? 👉👉👉👉 Next

Comments