
TaifaHouse
February 9, 2025 at 05:15 PM
*Ile ndoto tuliyoipa jina zuri la Pan Africanism imekwisha.*
Baba wa Taifa letu Nyerere, Kwame Nkuruma, Kenyatta, Samora, Kaunda, Sam Nujoma, Gaddafi na wengine, walibeba bara la Afrika kama nchi moja yenye nguvu.
Baada ya kupambana kutafuta uhuru wa nchi zote, kazi ya pili ilikuwa ni kuvunja mipaka ya wakoloni na kujenga umoja wa nchi za Afrika katika misingi ya Pan Africanism ambapo Mwl Nyerere alianza kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar wakati Kenya bado walikuwa wanajipanga. In fact Tanganyika na Zanzibar ilikuwa pilot kwa ajili ya mwendelezo wake ulitakiwa kusambaa nchi zingine za Afrika, kwa bahati mbaya athari za mabepari zilikuwa zimeshasambaa sana na hivyo haikuwezekana.
Viongozi wa karne ya sasa wamesahau kabisa mambo ya uafrika, wengi wanazungumzia utaifa, mipaka, maslahi ya kidiplomasia n.k zile harakati kama za #backtoafricamovement, Pan African Congress sasa ni historia
Pumzika kwa amani, Mzee Sam Nujoma. Wasalimie wapambanaji wenzako, waambie hali ni mbaya kuliko ilivyokuwa huko awali.