TaifaHouse
TaifaHouse
February 13, 2025 at 08:07 AM
*Wanaharakati mko wapi?* 1/3 Rais wa Marekani Donald Trump ametufungua macho, ameivua nguo Dunia. Ni baada tu ya kukata pesa za misaada ambazo nyingi zilikuwa zinasukuma agenda mbalimbali Duniani. Wanaharakati wengi ndio waliokuwa wanufaika wakuu kupitia fedha hizo wakitetea haki za binadamu na mazingira. Baada ya kukata minyororo ya kuwalisha wanaharakati, hatua iliyofuata ni kuwekea vikwazo mahakama ya kimataifa, ili mambo yake yasiingiliwe, wanasema mwenye nguvu mpe kazi awe busy, wakati mahakama ya kimataifa inapambana na vikwazo, Trump atakuwa ameshamaliza yake. Baada ya hapo ndo picha likaanza sasa, yaani hizi hatua ni za mtu anaejua vizuri anachokifanya. Baada ya kujitengenezea mazingira hayo, Trump alifanya kikao na Waziri Mkuu wa Israel, wakakubaliana kuichukua ukanda wa Gaza inayomilikiwa na wa-Palestina. Agenda ya Trump ni kuwaondoa watu kwenye nchi yao na kujenga mji wa kimataifa wa biashara. ...Inaendelea....

Comments