TaifaHouse
TaifaHouse
February 13, 2025 at 04:06 PM
*EAC Vs SADC na athari kwa Raila Odinga kuelekea Uchaguzi wa UAC* Zimebaki siku 2 uchaguzi wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AUC) ufanyike, presha inazidi kuwa kubwa kwa Mgombea pekee wa Afrika Mashariki Kiongozi kutoka Kenya Mhe Raila Odinga mwana wa Oginga Odinga. Baada ya nchi za Afrika zenye asili ya Arab kuonesha msimamo wao kumsapoti Mgombea kutoka Djibouti 🇩🇯 tumaini kuu la Raila lilibaki kwa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara. Kwa bahati mbaya pia nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zimetoa Tamko la nchi 16 kumuunga Mgombea kutoka Madagascar. Kabla ya hayo mabadiliko nguvu ya Raila ilikuwa kubwa akiongoza kati ya wagombea wenye nguvu, nchi za SADC zilitoa wagombea 2 mmoja kutoka Mauritius na mwingine kutoka Madagascar, aidha mgombea wa Mauritius aliyekuwa anategemewa zaidi akajiuzuru na kuacha kura zote za SADC kwa mgombea mmoja kutoka Madagascar. Ikumbukwe kwamba wakati Tanzania ni mjumbe wa SADC na Afrika Mashariki, Kenya sio mjumbe wa SADC. Katika nafasi hiyo, ni nchi za Afrika Mashariki pekee ndio hawajatwaa kiti hicho cha AUC, hivyo uchaguzi huu ulikuwa na makubaliano yasiyo rasmi ya zamu ya Afrika Mashariki. Aidha kufuatia mgogoro wa nchi jirani ya Congo, kumekuwa na mvutano kati ya umoja wa Afrika Mashariki na SADC iliyopelekea kufanya kikao cha pamoja nchini Tanzania. Mwenyekiti wa sasa wa Afrika Mashariki ni Rais wa Kenya Mhe Rutto ambaye pia ametoa matamko ya kimkakati kuhusu kutoa majeshi ya SADC nchini Congo na kurejea kwenye meza ya mazungumzo. Je hali hiyo itaathiri nafasi ya Raila kushinda? Je Raila aratoboa licha ya kuwa na kura zote za Afrika Mashariki? Je Afrika mashariki ina nguvu gani katika siasa za kikanda? Tanzania imefanya kampeni za kutosha kwa Raila Odinga na inamtakia kila la kheri katika uchaguzi wa Jumamosi.

Comments