TaifaHouse
TaifaHouse
February 16, 2025 at 03:46 PM
*Baadhi ya Visiwa Kufunikwa na maji* Tafiti zinasema kama mabadiliko ya tabia nchi yataendelea, mwinuko wa usawa wa bahari utazidi kuongezeka na hata kufunika kisiwa cha Zanzibar ndani ya miaka 100 ijayo. Tukiwa hapa Zanzibar, timu ilipata nafasi ya kutembelea mji wa zamani ambao unasemekana ulifunikwa na maji, mji huo upo katikati ya maji marefu lakini maji yake ni mafupi unaweza kushuka na kutembea ukikanyaga ardhi, inajulishwa kwamba katika eneo hilo maji yakipungua huwa inabaki ardhi ya kisiwa kilichozungukwa na maji ya kina kirefu kwa masaa kadhaa kabla maji hayajarudi kukifunika tena. Ni wakati sahihi wa kuhamasisha utalii wa ndani kwa watanzania, tujenge mazoea ya kutembelea na kujifunza kupitia vivutio mbalimbali nchini. *#zanzibarretreat* *#taifahouse*

Comments