
NURU YA UPENDO
May 20, 2025 at 05:59 PM
Matokeo ya swali letu tuliloluuliza;
*_Je! ulishawahi mvuta mtu hata mmoja kwa Kristo,?_*
Wengi wetu tumejibu ndio.. BWANA ni mwema sana.👏🏾
Lakini pia wengi wetu wamejibu *hapana* .. aidha kwa sababu ya hofu, uchanga, au kutokujua namna ya kuhubiri..
Ukweli ni kwamba injili haihitaji umahiri wa maandiko mengi, au ukomavu wa kiroho, au utashi...inahitaji kujiachia tu kutumika..Kwasababu ni asili ya Mungu kutumia vitu dhaifu kutimiza kusudi lake kamilifu (1Wak 1:27-28)
👇🏾
Anza kwa kusimulia ushuhuda wako na kile ambacho Mungu amekutendea ndani ya Kristo tangu ulipookoka..
Ukiwa unazungumza naye kwa maneno ya kawaida kabisa, huko huko katika mazunguzo, litazalika hili mara lile...hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu, endelea tu kuzungumza habari za Mungu kwa maneno ya kawaida hivyo hivyo..mpaka utajikuta unamweleza maneno ambayo si wewe kwa namna ya kawaida ungeweza kuwaza vile...
Usitegemee tu akili zako sana, wala usifikiri-fikiri...ukipita njiani, ukiwa shuleni, kazini, nyumbani...anza...kwa urahisi kabisa..Bwana atakusaidia kufundisha. Ukiokoka leo, una nguvu sawa na yule aliye ndani ya Kristo kwa miaka mingi katika eneo la ushuhudiaji. Hivyo usiogope
Lakini ikiwa bado hujaokoka na unajitaji msaada huo wa kumpokea Yesu, ili na wewe akupe Roho wake kukusaidia kuwashuhudia wengine..basi wasiliana nasi kwa namba hizi👇🏾
+255693036618 / +255789001312
www.nuruyaupendo.com
🙏
❤️
❤
👍
😢
27