
Nukta Habari
May 16, 2025 at 08:52 AM
Dar es Salaam. Kampuni ya huduma za simu ya Vodacom Tanzania imetangaza ongezeko la faida baada ya kodi la zaidi ya Sh37 bilioni ndani ya mwaka mmoja na kufikia Sh90.5 bilioni katika mwaka wa fedha ulioishia Machi, 2025 ikichochewa zaidi na kuongezeka kwa mapato ya huduma na mkakati wa kuminya matumizi.
Ongezeko hilo la faida ni habari njema kwa wawekezaji wa kampuni hiyo ambao wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuongezeka kwa gawio ili kutunisha zaidi mifuko yao.
https://nukta.co.tz/vodacom-tanzania-yaripoti-faida-ya-sh90-5-bilioni
❤️
1