Economist SHILLA Jr.
May 27, 2025 at 05:52 AM
KILA SIKU JIULIZE MASWALI KUMI (10) ILI UWEZE KUTAFAKARI NA KUAMUA KUWEKA MIKAKATI THABITI ILI USONGE MBELE KIFIKRA NA KIMAENDELEO: Katika maisha kuna maswali mengi tunapaswa kujiuliza mara kwa mara kwa ajili ya kutafakari na kujitathmini wenyewe kwa lengo la kusonga mbele kimaendeleo. Leo nimepata kibali cha kukuletea maswali kumi (10) ambayo kwa namna moja au nyingine ukitumia muda wako kujiuliza, kutafakari na kutafuta majawabu basi yatakusaidia kupiga hatua moja mbele kifikra na kimaendeleo. Maswali haya ni kama ifuatavyo; 1. Je, tabia zako za kila siku zinakusaidia katika kusimamia pesa zako vizuri katika uwekaji wa akiba na uwekezaji au ni chanzo cha kufuja na kutapanya pesa hovyo? 2. Je, unafahamu unahitaji kiasi gani cha fedha kwa ajili ya matumizi yako kwa kipindi cha mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita au mwaka mzima? 3. Je, unajua fedha (kipato) zako unazoingiza kwa mwaka mzima huwa zinatumika wapi na kiasi gani kinatumika katika maendeleo na kiasi gani kinatumika katika matumizi ya kawaida? 4. Je, unaweza kurejea katika hali yako ya sasa kwa haraka (uhimilivu) kipindi unapopatwa na matatizo au changamoto za kifedha? 5. Je, umewahi kujiuliza, marafiki na jamaa waliokuzunguka ni faida au hasara kwako?. Wanakusaidia kuongeza kipato au kuongeza matumizi na madeni? 6. Je, kiwango cha akiba ya fedha ulichonacho kinatosha kuendesha maisha yako kwa kipindi cha miezi mingapi iwapo utakosa kazi ya kukuingizia kipato, mfano umeachishwa kazi n.k? 7. Je, kiwango cha madeni ulichonacho ni himilivu au madeni yamesababisha kutoaminika kwa marafiki na ndugu zako?. 8. Je, mwenza uliyenaye ni chanzo cha migogoro ya kifedha ndani ya ndoa au yeye ni msaada mkubwa katika usimamizi wa fedha ikijumuisha matumizi mazuri ya fedha, uwekaji akiba na uwekezaji? 9. Je, unapoenda kufanya manunuzi ya bidhaa sokoni unatumia mbinu gani ili uweze kununua biadhaa unazohitaji kwa bei nafuu na kwa kuzingatia mahitaji halisi au unapoenda sokoni unanunua bidhaa chache kwa bei kubwa au ukanunua bidhaa usizozihitaji kwa wakati huo. 10. Je, mali ulizonazo iwe fedha, nyumba, viwanja, mashamba n.k zinafikia thamani ya kiwango gani? Je kwa sasa unao utajiri (net worth) wa kiwango gani ukitoa madeni uliyodaiwa? Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].

Comments